Friday, February 23, 2018

MTU AMBAYE HUTAKIWI KUMTILIA MAANANI

"Imani ni kama mbegu. Inakuhitaji kukumbuka kwamba mbegu hainenepi wala haikondi bali inakua, licha ya hivyo vyote mbegu lazima uipande, uiwekee mbolea, uipalilie na kuwa na uangalizi mzuri kutokushanbuliwa a wadudu n.k ili iweze kuzaa matunda bora zaidi. Hata wewe lazima uwe na imani ya mafanikio, ni lazima uhakikishe unaipanda mbegu ya imani na kuifanyia kila kitu ili baadae ikupe matokeo mazuri zaidi.Cha msingi zaidi kumbuka Imani bila matendo si kitu."

Mtu ambaye hutakiwi kumtilia maanani sana katika maisha yako;

1. Mtu ambaye anapenda  kazi au shughuli yako zaidi ya wewe. Huyu ni mtu ambaye atakupenda au atakuona wa maana ukiwa na kitu lakini ukikikosa kwake thamani huna tena, sio vyema kujitoa kwake sana wala kumpatia muda wako.

2. Mtu ambaye anashindana nawe kwa nia ya kutaka kuwa juu yako kwa kitu unachokifanya. Mashindano hayakatazwi kwasababu  huwa yanaonesha ubora wa mtu lakini mashindano bora yenye kuonesha ubora bora ni ule unaomfanya mtu kushindana na yeye mwenyewe kuwa bora.

3. Mtu anayetaka kuchuma vyako tuu badala ya kujifunza katika uchumaji wako na yeye ajue jinsi ya kuchuma vyake. Mtegemea cha nduguye hafi mwenyewe masikini lakini hata yule anayembweteza hufa masikini pia.

4. Mtu ambaye anajiona anajua kila kitu.Huyu ni hatari kwasababu hauwezi kushauriana naye wala kubadilishana nae mawazo, kila kitu atakuwa anajiona sahihi na wewe hata kama utakuwa sahihi mawazo yako yatashushwa chini na kuonekana sio kitu. Muda mwingi  hawa huwa ni wakatisha tamaa na wabinafsi kimawazo muda mwingine kimatendo kabisaa😀.

5. Mtu anayependa kufanya wenzake wafuasi wake bila hata kuwafundisha chochote ambacho kutawasaidia na wao kuweza kupandikiza mbegu bora kwa watu wengine.

6. Mtu asiyependa kuwa kichocheo cha mabadiliko yoyote. Hawa utakuta kila unachotaka kubadilisha wenyewe hupinga tu hata kwa sababu ambazo zinaonekana wazi wazi hazina uzito wowote.

n.k

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi
#MwongozoKatikaMafanikio

0 comments:

Post a Comment