Saturday, January 6, 2018

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KWA MWAKA 2018

Habari mpenzi msomaji wa mtandao wetu wa Lazaro Samwel, naimani unaendelea vizuri na majukumu yako ya kawaida. Nazidi kukwambia kwamba mwaka huu ni mwaka wa baraka katika maisha yako tofauti na miaka mingine iliyopita.

Kuna mambo muhimu ambayo leo hii nimeona nikushirikishe kuweza kuhakikisha kwamba kwa mwaka 2018 unaenda vizuri na unakuzalia matunda mazuri katika maisha yako.  Inawezekama miaka nenda rudi huwa unaishia sehemu moja tuu na hauoni mabadiliko yoyote katika maisha yako lakini leo hii nitakuelekeza mambo ambayo unatakiwa kuzingatia ili mwaka 2018 uweze kuwa wa kitofauti na miaka mingine ambayo imepita.

Mambo hayo ni yapi ambayo unatakiwa kuzingatia au unatakiwa kuyabadilisha kwa mwaka huu wa 2018, kumbuka siku zinaenda na hazikusubiri kwahiyo inabidi pia na wewe ukubali kwenda na muda kweli;

1. Badili aina ya kazi au utendaji wako wa kazi kama zinakupa matokeo yale yale miaka nenda rudi.  Hapa kuna mambo mawili kwamba unaweza kuwa unafanyabkazi nzuri tatizo likawa kwako katika utendaji wako wa kazi na isikuletee matunda mazuri na kuna kazi ambayo kwako inaweza isiwe sahihi licha ya wewe kuwa na utendaji wako mzuri wa kazi. Angalia katika mambo haya mawili na kumbuka kwamba ukitaka mabadiliko lazika ukubali kubadilika na sio kujihurumia kubadilika, kama itakuhitaji wewe ubadilike hakikisha kweli unabadilika na kama kweli itakuhitaji ubadili kazi hakikisha unabadili hiyo kazi ili usipoteze muda.

2. Acha matumizi ya sehemu ambazo sio muhimu. Acha starehe ambazo hazina umuhimu, acha kununua nguo bila sababu muhimu, acha kununua simu gharama bula umuhimu wowote,  acha kwenda kustarehe na marafiki zako bila umuhimu wowote n.k hela ambayo ungeipoteza sehemu hizi ambazo sio muhimu jitahidi mwaka huu 2018 unaweka akiba kuwekeza katika biashara au hata ukafanya utaratibu kununua kiwanja.

3. Kuwa na uchaguzi mzuri wa marafiki kwa mwaka huu 2018, angalia kuongeza marafiki ambao watakuwa na mchango chanya katika maisha yako na ondoa marafiki ambao hawana mchango wowote katika maisha yako. Usionee mtu huruma kwasababu mwisho wa siku unatakiwa kutimiza jambo flani katika maisha yako.

4. Jitahidi sana kuwa mtubwa matendo mwaka huu kuliko kuwa mwongeaji sana, usibishane na watu na wala usitake kujionesha wewe ni bora zaidi ya wengine, acha matendo yako yakuseme wewe bila hata kutumia nguvu sana. Talk less do more.

5. Tumia mitandao ya kijamii kwa mambo ambayo ni ya msingi,  kama mwaka 2017 mitandao ya kijamii haikuchangia chochote katika maisha yako zaidi ya kuperuzi tuu kufuatilia maisha ya wengine,  kuchat mambo ambayo sio ya msingi basi mwaka 2018 ufanye uwe wa kitofauti kwa kuhakikisha kwamba mitandao ya kijamii inakunyanyua katika nafasi zingine katika uwezo uliokuwa nao,  kama ni biashara basi hakikisha unaitangaza,  kama unakipahi cha mpira hakikisha kwamba unajitangaza,  kama ni mwimbaji pia hakikisha watu wanakujua kwa kile unachokifanya kama ni mpishi hakikisha watu wanatambua huduma yako.  Mitandao ya kijamii ndipo watu walipo sasahivi kwahiyo usiikimbie.

6. Hakikisha kika unachokifanya kinakuwa ndani ya hatua za kutumiza malengo yako na sio nje ya hapo,  kama bado ulikuwa hujaweka malengo au hujaandika pembeni unataa kutumiza nini kwa mwaka 2017 hakikisha unaandika mapema na jinsi ya utakavyokuwa unachukua hatua kika siku taratibu ili uweze kuyafikia. Acha kuishia maisha ya kutabirika mana hata matokeo yako yatakuwa ya kubahatisha tuu.  Badilika ndugu yangu.

Naimani kuna kitu ambacho umekipata katika somo hili,  share na mwenzako lakini pia unaweza kuacha comment chini kwa ulichokelewa au kwa nyongeza pia.

JITAHIDI SANA KUPATA VITABU VYA AKILI YA USHINDI kama kitabu cha BIASHARA NA UJASIRIAMALI unatakiwa kuwa nacho lakini pia unatakiwa kuwa na kitabu cha SAFARI YA MAFANIKIO kujua jinsi unavyoweza safiri vizuri kuelekea katika mafanikio yako. Vyote unavipata kwa 23,000/= tuu.

Ulikuwa nami;

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
Email;  lazaro@akiliyaushindi.com


0 comments:

Post a Comment