Sio kila unachomasishwa unatakiwa kukifanya, unatakiwa kuwa makini sana katika hili kwasababu unaweza shangaa unapoteza muda na kuja kumlaumu yule aliyekuhamasisha au kukuelimisha.
Ni jambo la busara sana kuwa makini sana na kujichunguza ndani kwa kujiuliza je nilichohamasishwa au ninachohamasishwa kukifanya jee ni jambo ambalo liko ndani ya wangu ? yani unalipenda kwelii au ni kwasababu tuu umepata hamasa muda ule kulifanya ?
Hii inanikumbusha wakati nafanya Network Marketing Business watu waliokuwa wakihudhuria katika semina yaani Business Opportunity Meeting wengi walikuwa wanaingia au kuchukua maamuzi ya kufanya biashara kwa hamasa tuu ya kuona mtu flani kapata kitu flani na sio wao wenyewe kutoka ndani yao kuwa na nia ya dhati kufanya hiyo biashara. Mwisho wa siku unakuta kuna malalamiko mengi sana kwa watu ambao unakuta waliwaingiza watu hao.
Utasikia, "Wewe uliniambia hivi ndio maana nikaingia kuifanya biashara hii." hapo unakuta kwasababu ya biashara kuwa na changamoto flani licha ya mara ya kwanza kuambiwa biashara hii iko vipi.
Nachotaka kukwambia ni kwamba hisia zinaweza kukufanya kufanya maamuzi ambayo sio sahihi pale unapokuwa na hamasa kwahiyo jitahidi akili yako isifungwe na hisia za hamasa yako na kuwa na nafasi ya kufikiri kabla ya kutenda katika kile unachohamasishwa.
Sio kila anayekuhamasiaha yupo sahihi na wala sio kila unalolisikia ni kwaajili yako kuwa makini na pembua mambo kwa umakini.
Kocha Lazaro Samwel
0753616584

0 comments:
Post a Comment