Tuesday, May 8, 2018

KWANINI UNATAKIWA KUSONGA MBELE KWA KILE UNACHOKIFANYA ?


" Mdomo wako unaweza kutamka kutaka mafanikio lakini maisha yako yakakana uliachozungumza na kukinena kwa watu. Ulipewa mdomo mmoja, miguu miwili,  masikio mawili,  mikono miwili  na akili ili utende kwanza kuupa mdomo wako uhakika wa kuongea kitu sahihi, hakikisha unavitumie ipasavyo kabla ya mdomo wako." - Lazaro Samwel


1.  Songa mbele kwasababu kitu chako hakijakubeba wewe tuu tambua katika shughuli yako kuna ndoto za watu wengine pia umezibeba kuweza kutimia.

2. Songa mbele kwasababu sio kila mmoja ambaye anapenda kusaidia wengine kama wewe unavyofanya unachokifanya.

3. Songa mbele kwasababu inawezekana ile historia mbaya katika uzao wenu wewe ndiye unatakiwa kuibadilisha mfano inawezekana watu wanasema katika familia yenu hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa,  inawezekana pia toka zamani mlinenewa kwamba maisha yenu hayawezi kubadilika. Wewe unaweza kuwa mkombozi.

4. Songa mbele kwasababu kuna alama unatakiwa kuiacha katika uso wa dunia hii na katika uzao wako na alama hiyo sio ya kusahaulika.

5. Songa mbele kwasababu hata yule anayekwambia kwamba huwezi anahitaji msaada wako kupitia mafanikio yako. Kuna watu wameshakata tamaa na maisha na wewe wanakukatisha tamaa kwasababu wao walishashindwa sasa mafanikio yako yanaweza kuwa chanzo cha wao kubadilika na kuona kumbe inawezekana.

6. Songa mbele kwasababu suluhisho la changamoto au matatizo yako sio kuacha unachokifanya au kukata tamaa, suluhisho ni kusonga mbele na kushinda au kufanikisha malengo yako bila kutazama maumivu yako.

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi

0 comments:

Post a Comment