Tuesday, May 8, 2018

UNATAKIWA KUFANYA NINI KWA WALE WANAOTUMIA MAPUNGUFU YAKO KUKUSEMA VIBAYA ?



" Hapa duniani kuna makundi 2 ya watu ;

1. Kundi la Albert Einstein - Hawa ni watu ambao wana maono na mawazo ya mbali lakini watu wengi hawawaelewi na inawezekana wanaonekana kama hawana akili na wamechanganyikiwa kwa sasa. Inawezekama kuna watu wanawaelewa lakini hawaamini kwasababu wengi wanasema hawapo sahihi lakini naimani kuna siku wataeleweka na watu watasema walikuwa sahihi.

2. Kundi la Charlie Chaplin ;  Hawa ni watu ambao wanafanya mambo kwa ukimya hawana maneno sana na ni wachache sana wenye akili ya kufikiri pia huwaelewa wanafanya nini lakini kuna wengine wanaona kwa ukimya wao kitu wanachokifanya hakieleweki na hakina maana yoyote kwa wakati huu.  Naimani watakaposonga mbele na kuamini wanachokifanya kuna wakati watu watawaelewa." - Lazaro Samwel

Usiache hata siku moja mtu kutumia mapungufu yako kuwa kama gia ya kupata kuongea kwa wengine na wewe kufanya makosa yasiyokuhusu. Wala usiruhusu mtu kutumia kushindwa kwako iwe sababu ya kupata mada ya kuongea katika makundi ya watu na kuonesha kwamba wewe sio kitu na yeye ni kitu.

 Kivipi sasa unaweza kufanya hivi ?

1. Usibadilike kwa maneno yake ya kujaribu kukushusha kama mwendo ulikuwa wa mbele basi amka na songa mbele.

2. Usitumie na wewe muda wako kwenda kuongea na watu kuhusu ubaya wa huyu anayekusoma , wewe piga kazi na kazi yako ndiyo iongee kwa wale walioambiwa kuhusu kuanguka kwako au mapungufu yako.

3. Usiwachukie wale walioambiwa wala yule aliyewaambia, show love and be real kwasababu ukweli haujifichi na haufichi kweli yake na uwongo haujifichi kuonesha uwongo wake.  Mwisho wa siku itajulikana kipi ni kipi na nai alikuwa mbaya.

4. Usipoteze muda wako kuwaza kwanini amewaambia wengine kuhusu kuanguka kwako au mapungufu yako kwasababu kilichoongewa hakiwezi kurudishwa tena mdomoni na maneno ya uwongo hupingwa kwa matendo. Wekeza muda wako katika kujifunza kwenye kuanguka kwako, wekeza muda wako kwenye kujifunza jinsi ya kwenda sawa na mapungufu yako yani ujue wapi uongeze uimara na sio kuwa mkamilifu.

Enjoy Your Day.

Kocha Lazaro Samwel
0753616584 or lazarosamweli41@gmail.com
#akiliyaushindi

0 comments:

Post a Comment