Habari mpenzi msomaji wa makala hizi katika mtandao wa Lazaro Samwel naamini unaendelea vizuri ba majukumu yako ya funga mwaka.
Leo hii katika kipengele hiki kuna mambo machache ambayo nitajitahidi kukuorodheshea kuweza kuzingatia kwamba unayabadili au kuyaacha unapojiandaa kuingia mwaka wako mpya 2018.Mambo haya yanaweza yasiwe mageni kwako lakini ni kwa nia ya kuendelea kukumbushana na kutilia mkazo kwa sababu wote ni wanafunzi na hakuna mkamilifu wa kusema kwamba hataki kukumbushwa au kujifunza.
Mambo hayo kwa orodha ambayo unatakiwa kuhakikisha kwa mwaka huu kwa hizi siku chache zilizobaki unatakiwa kuhakikisha kwamba unayabadili au kuyaacha ni kama ifuatayo;
1. Badilisha aina ya marafiki ambao inawezekana kwa mwaka 2017 hawakupa changamoto yoyote ya kukufanya kutimiza jambo flani katika maisha yako na mwisho wa siku ukaishia kujuta.
2. Acha kusoma mambo ambayo hayana msingi katika maisha yako haswa kama kwa mwaka 2017 ulitumia muda wako kusoma mambo ambayo sio ya msingi jitahidi kuachana nayo mfano magazeti ya udaku ambayo unakuta hayachangii chochote katika maisha yako, vitabu vya kukufurahisha tuu lakini havina funzo lolote ndani yake n.k
3. Badili tabia yako ya kulalamika katika kila jambo ambalo linatokea katika maisha yako kwasababu utafunga na uwezo ambao ungeweza kuutumia kuweza kuhakikisha unachokilalamikia unakishinda.
4 Badili matumizi yako ya hela mfano kama ulikuwa huweki malengo jitahidi sasa hiyo tabia unaiacha na mwaka 2018 unavyoingia uwe na malengo pamoja na kujenga tabia ya kuweka akiba katika kile ambacho unakipata.
5. Acha tabia ya uwoga, mbegu hii hakikisha unapoingia mwaka 2018 uwe umeshaingoa na kupanda mbegu ya ujasiri wa kuthubutu katika mambo ambayo ulikuwa unayaogopa.
6. Acha tabia ya kutokumshirikisha Mungu katika mambo ambayo unayafanya.Jitahidi mwaka 2018 unavyoingia Mungu awe katikati ya mambo yako na katika maamuzi yoyote ambayo unataka kuchukua hakikisha unanena naye kwa Sala na Imani.
7. Acha tabia ya kutamani kuwa kama watu flani, jikubali na amini mawazo uliyokuwa nayo bila kuhofia nani na kuangalia ukifanya unachotaka kukifanya.
8. Acha tabia ya kuwa na uvivu wa kusoma vitabu maana huku ndipo penye majibu mengi ya maswali ambayo unajiuliza katika maisha yako.Kwahiyo jiweke malengo ya usomaji wa vitabu kwa mwaka 2018 unaingia anza taratibu katika kujenga tabia ya usomaji, andaa kwanza vitabu ambavyo unahisi vitakusaidia kuanza kujenga tabia ya usomaji kwa kuzingatia unapenda maswala gani, jiwekee target ya usomaji wa kurasa kila siku na kadri siku zinavyosogea endelea kujiongezea idadi.
Nyongeza: Badili au achana na mahusiano ambayo hayana maana yoyote katika maisha yako, jitahidi kuwa na mtu ambaye anamaana katika maisha yako na wewe unamaana katika maisha yake, kuwa na mahusiano ambayo yana kuwa na mwelekeo na makubaliano ya kitu ambacho mnafanya wote au mtu mmojawapo kati yenu.
➡ Mahusiano ambayo yapo kimaslahi au kwaajili ya kujionesha mmojawapo kuwa bora zaidi ya mwingine hayo sio mahusiano ambayo unatakiwa kuwa nayo.
➡Mahusiano ambayo mtu ana wivu kwa juhudi za mwenzake hayo sio mahusiano ya kuendelea nayo.
➡ Mahusiano ambayo mnakuwa busy katika shughuli zingine ambazo unakuta muda mwingine zinakosesha muda wa mambo yenu binafsi au zinasababisha mwingine kuleta dharau kwa mwenzake haya sio mahusiano ya kuendelea nayo.
➡ Mahusiano ya kutaka kua kama watu flani na sio nyie kuwa nyie (mahusiano ya tamthilia) achana nayo angalia kuwa na mtu ambaye atataka nyie kuwa kama mlivyo kwa kujiboresha zaidi, mahusiano ambayo hayana usikivu wa kurekebishwa au kurekebishana sio mahusiano ya kusonga nayo mbele.
Ungana na wenzako 100 katika program yetu mpya ya AKILI YA USHINDI kwa kuchukua vitabu 2 (BIASHARA NA UJASIRIAMALI na SAFARI YA MAFANIKIO) kwa 23,000/=, unapopata vitabu hivi utapata nafasi ya kuwa katika group la whatsapp kwaajili ya kunufaika na mafunzo ya miezi 3 mwakani, utapa coaching and mentoring kutoka kwa Kocha Lazaro Samwel kupitia simu yako ya mkononi na hata muda mwingine kukutana uso kwa uso kama unaweza kuwa karibu yake au akiwa yupo maeneo yako ya karibu.Bonyeza link hii kupata maelezo zaidi juu ya program hii ;https://akiliyaushindi.com/
Ulikuwa nami;
KOCHA LAZARO SAMWEL
0753616584
EMAIL; lazaro@akiliyaushindi.com

nakuelewa sana kaka team success kingdom
ReplyDeleteKaribu sana kileo Seif.
ReplyDelete