Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel, naimani unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku na nina kila sababu ya kumshukuru Mungu Kwa uzima wako ulikuwa nao Kwa siku hii ya leo.
Lakini kabla ya kuanzia ningependa kukwambia kwamba kujua kusudi lako ni chimbuko la kufanya kitu ambacho unakipenda na ndio maana sio kazi rahisi kujua kusudi lako kama ilivyo kazi kujua kitu ambacho unakipenda kukifanya katika maisha yako.Inahitaji mtu mwenye nia ya dhati kabisa kutoka moyoni kujisaka kwanza ndani yake.Kusudi lako tunaamini kwamba limebeba kila kitu ambacho kinahitajika katika maisha yako.
Mambo gani ambayo unatakiwa kuyafanya kutambua au kupata kitu unachokipenda?
1. Kwanza jiulize kitu ambacho unakifanya sasahivi unakipenda au hukipendi kama hukipendi haina maana yoyote ya wewe kuendelea kukifanya ikiwa unajua kabisa kwamba hakuna mafanikio yoyote ambayo mtu unaweza kuyapata katika jambo ambalo halina upendo wako.
2. Kama kitu ambacho unakifanya sasahivi haukipendi jiulize ni vitu gani vingine ambavyo unavipenda kutoka moyoni mwako? Chukua kalamu andika pembeni mambo yote ambayo unayapenda,anza na kile ambacho unakipenda zaidi mpaka kile ambacho unaona ni cha mwisho.
3. Chukua muda kuwaza kwa kila kitu ambacho umekiandika kwa kujiangalia pia wewe mwenyewe na uwezo wako jambo uwezo wako hauna kikomo. Hapa unachotakiwa kukifanya ni kuangalia nguvu na mapungufu ya kila kitu ambacho umekiandika sambamba na kuangalia pia uwezo wako na mapungufu yako yalipo.Usije ukasahau hapa ni sehemu ambayo unaweza kuchukua muda kwasababu muda mwingine itakubidi kuweza kufanya uchunguzi au kukutana na watu ambao ji wazoefu katika pande zile za vitu ambavyo umekiandika.
4. Chukua vitu 5 bora ambavyo baada ya kuvifikiria ukaona kwamba in bora zaidi ya vitu vingine.Katika zile tano unatakiwa kupata kitu kimoja ambacho ni bora zaidi.Katika vitu hivyo 5 ambavyo utakuwa umechagua sio mbaya pia ukaangalia kila wazo mapungufu na nguvu yake,na hii itakuhitahi uwe umefanya vizuri katika hatua ya 3 na uwe unaelewa kila kitu katika nguvu na mapungufu yake.
5. Chukua kitu kimoja bora zaidi na mambo 4 yanayobaki yatunze. Baada ya kupata kitu hiki kimoja ni vema ukatafuta majibu ya haya maswali;
~Uko tayari kuanza kufanyia kazi jambo hilo?
~Utalifanyiaje kazi jambo hilo? Utatumia nini au vifaa gani au watu gani utajumuika nao jambo lako liweze kusonga mbele.
~ Mahali gani ambako unapenda kitu chako kianze kufanyiwa kazi?
BAADA YA HAPO UNAWEZA SASA KUCHUKUA HATUA KUKUTENDEA KAZI JAMBO LAKO.
N.k
JITAHIDI KUJISAJILI KATIKA PROGRAM ya http://www.akiliyaushindi.com/jiandikishe kuna mengi ambayo unatakiwa kujifunza zaidi katika program hii ya mwaka mmoja. Bonyeza hiyo link na hata maelekezo zaidi.
Ulikuwa nami;
Kocha Lazaro Samwel
0753616584
Email; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:
Post a Comment