"Heshima yako utaanza kuijenga kwa kujiheshimu mwenyewe na kuheshimu wengine kwanza"
Kuna mambo ambayo watu huwa wanayafanya bila kujua kwamba wanashusha thamani zao.Tena mwingine huendelea kuyatenda mambo hayo na kumfanya kumjengea tabia kabisa katika maisha yake.Heshima yako ni kama chapa yako,heshima yako ndio biashara yako,heshima yako ndio msingi mzuri wa maisha yako na ya wazazi wako.
Leo nitaenda kukushirikisha baadhi ya mambo machache ambayo ya kusaidia kulinda heshima yako;
1. Chunga kinywa chako kujua wapi unatakiwa kuongea,nini unatakiwa kuongea, kwa watu gani unatakiwa kuzungumza nao na ni kwa muda gani.Kinywa chako kunena mambo ambayo ni ya ukweli na kwa watu ambao ni sahihi au hata kama sio sahihi inajenga heshima yako lakini kinywa chako kunena maneno ya uwongo kwa watu ambao sio sahihi kwa uwongo wako patashusha heshima yako na hata kwa wale ambao ni sahihi kwa uwongo wako watakusikiliza lakini jua hata wao hawatakuheshimu hata kidogo.
2. Jitahidi muda wako kutumika katika mambo muhimu katika jamii.Mfano katika misiba ya watu wengine jitahidi kuhudhuria mikutano ya kijamii, changia kimawazo na hata katika mambo ya kifedha sehemu zenye uhitaji,ungana na watu katika michezo ya kijamii.
3. Usipende kuwa mtu wa kuwa na malalamiko katika kila jambo ambalo linatokea katika jamii yako.Kuna watu ambao wanatumia mitandao ya kijamii kulalamika hii tabia acha maana unazidi kushusha heshima yako na hata utafanya kudharaulika.
4. Tumia kipaji chako kuinua wengine au kufanya wengine hata kuwa zaidi ya wewe katika maisha yao.Nakuhakikishia heshima yako itakuwepo hata siku utakapoondoka hapa duniani.
5. Penda kusikiliza watu zaidi kuliko kuongea sana nawe utawaweka karibu nawe na watakuheshimu kama wao watakavyoona unawaheshimu kwa kuwapa muda wako kuwasikiliza.Ukipenda kuongea sana hata kabla ya kumsikiliza mtu unashusha hadhi yako kwa asilimia kubwa.
6. Fanya unachokipenda hata kama hakuna mtu anayefanya kitu kinachofanana na unachokupenda.Huko ndipo utakapojenga heshima yako na watu watakuheshimu,ukisema uwe kama mtu mwingine hautaweza kuheshimiwa kwasababu unachokifanya heshima yake imeshaenda kwa anayepaswa kuheshimiwa kwa anachokifanya.
7. Heshimu familia yako haswa wazazi wako kwanza, unavyoonesha heshima kwa wazazi wako ndivyo hata watu wengine watakuchukulia katika kukuheshimu. Lakini pia heshimu ndugu jamaa na marafiki hawa ndio watu muhimu sana kwako katika kukusema kwa mema yako na watu wengine watajua kwamba unajiheshimu na unatakiwa kujiheshimu pia.
Naomba kuishia hapo,najua kuna mengi ambayo unapenda kujifunza hakikisha kwanza unajiunga na program ya akili ya ushindi kwa kubonyeza http://www.akiliyaushindi.com/jiandikishe huku utapata maelezo yote pamoja na utaratibu wa kuwa mwanachama kamili. Karibu kufanya kazi nami kwa mwaka 1 kwanza.
Ulikuwa nami;
Kocha Lazaro Samwel
0753616584
EMAIL; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment