BADILI AKILI,ONA FURSA,BADILISHA MAISHA YAKO.
Jambo lolote kubwa duniani ambalo unakiona Leo ni matokeo ya mambo mawili;
1.Makosa
2. Kushindwa
Hakuna jambo Leo ambalo utataja mafanikio yake bila kutaja haya mambo mawili ,angalia matajiri wote wakubwa duniani na hata wale ambao wanaibukia wote simulixi zao za mpaka walipofika ni kwasababu ya kutambua uwepo wa haya mambo.Hivi unadhani Thomas Edson angeendelea kuongopa makosa na kushindwa kwake kwa mara ya kwanza kutengeneza balbu Leo hii tungeweza hata kuwa na mwanga wa balbu,Wright Brothers wangeondoa imani kwao kwasababu ya makosa na kushindwa kwa Mara ya kwanza KUTENGENEZA ndege unadhani Leo tungekuwa na Air Tanzania,fly Emirates,Air Tanzania na ndege za mataifa mengine kuna watu wengi sana ningependa na wewe uangalie wale ambao wako mtaani kwao au katika ncho yako waulize historia yao ya mafanikio au mpaka pale walipofika nakuhakikishia 99% ya ambao utawaulizia lazima watataja makosa yao na watataja sehemu ambazo waliwahi kushindwa lakini wakasonga mbele.
Nataka nikusihii wewe ambae unasema 10,000/= haiwezi kuwa na msaada wowote kama mtaji hela umuulize msukuma au mtu yoyote ambaye yupo Mwanza ananunua kisado 1 cha dagaa na kuwafunga vizuri kusafirisha mikoani anatalengeneza shilingi ngapi sasa kama yupo serious na biashara, wewe mwenye 50
60,000/= au hata chini ya hapa muulize mtu aliyeanza na kuku 5 au 4 tuu kufuga na Leo hii yuko ? Muulize mama aliyenza na mtaji wa 20,000/= KUTENGENEZA barafu za kawaida Leo hii yuko wapi? Hebu Leo toka na Akili yako uliyonayo na hela yako ndogo ambayo unaidharau ipe heshima yake kwa kujifunza kwa wengine wameweza kuanzaje biashara ndogondogo,usidharau udogo wa biashara flani ukadhani huwezi kufika kimaisha,nakusihi jifunze tuu hata kaka ni ndogo. Udogo huu ndio ambao unaweza kukuletea baraka tela za kufanya mambo makubwa.Elimu yako isikuchagulie fursa ya kufanya wewe ndiye unayetakiwa kuchagua ,cheti chako kisiwe chanzo cha kuchagua fursa utakufa masikini ndugu.
Hebu acha visingizio Leo amka na tafuta jambo ambalo utaanza nalo hatua ndogo hata kama Leo uko katika huzuni ya namna gani,nachomaanisha upate kitu ambacho kitakufanya usogee sehemu katika maisha yako. Nitapenda siku moja unisalimu kwa kuniambi Kocha Lazaro Samwel nimeanza kitu flani Nashukuru au nimeweza fikisha kitu changing sehemu flani.
Naamini wewe ni mshindi na Una Akili Ya Ushindi.
Kama bado hujajiunga na program ya akili ya Ushindi hakikisha unajisajili ili uweze kupata masomo mengine kabambe yatakayokusaidia katika maisha yako.Kupata maelezo zaidi Click http://www.akiliyaushindi.com/jiandikishe
Ulikuwa nami;
Kocha Lazaro Samwel
0753616584
Email; lazarosamwel

0 comments:
Post a Comment