Skip to content
"Kobe hujongea mbele pale anapotoa kichwa chake nje na sio kichwa chake kinapokuwa ndani"
Maisha yako hayataweza kusonga mbele ukiweka uvivu katika kutumia akili yako.Ukitaka maisha yako yaweze kubadilika acha tabia ya kuangalia chini kwa kutokutumia akili yako katika mambo sahihi katika maisha yako kwa maana utakavyoangalia chini utapata unachokitaka na kitakuwa sio sahihi mana ulipoangalia sio sahihi pia. Kobe kutoa kichwa nje kiuhalisia ni kwamba kichwa kukaa ndani hawezi kufika anapopataka,naweza kusema kutoa kichwa nje kwa kobe ni hekima ya kuweza kujua kwanini kuweka kichwa ndani hakuna manufaa katika kutimiza lengo lake. Binadamu pia kutokutumia akili zetu ni sawa na kobe ambaye ameweka kichwa ndani na tunapochukua jukumu la kuweza kutumia akili zetu ni kama kobe anavyotoa kichwa nje.Hebu jiulize ni mara ngapi unakutana na mambo ambayo yanakufanya usitumie akili yako na kwelii hutumii? Jiulize kuna faida gani kulalamika kwamba maisha magumu ukiwa hata chembe ya akili yako unaogopa kutumia? Unadhani ni haki kwa wewe kuweza kuishi maisha haya? Hebu chukua hatua kwa majibu ambayo unajipatia.
Lazaro Samwel
Life Coach
0753616584 / 0653386586
Email ;lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment