Saturday, August 26, 2017

SIRI YA KUANZA UNACHOKIPENDA

"Kitu Chenye Upendo Ndani Yake Tiba Ni Kuanza Kukifanya" - Lazaro Samwel

Kuna njia moja nzuri ya kunawirisha unachokipenda kukifanya na njia hiyo ni kuanza kukitumia kile unachokipenda kwa wengine acha kukiwazia sana kupita kiasi.Nikwambie kitu kimoja, kuwaza au kufikiri kupita kiasi  kufanya kitu unachokipenda ni kujenga msingi wa uwoga.Upendo ulipo katika jambo flani ni gia namba moja ya kuanza kupiga hatua nzuri.Leo hii umekaa unapenda kufanya biashara flani akilini mwako unawaza biashara ya 1,000,000/= lakini una laki 5 alafu unaacha kufanya kwasababu haijafika hiyo milioni 1, kwanini usianze na hiyo laki 5 katika biashara yako ambayo inahitaji mtaji wa milioni 1? Kuna watu wana 10,000/= tuu na wanaanzisha biashara baada ya mwaka mmoja anamtaji unaongezeka mara 100 ya alioanza,wewe unasubiri nini?

Akili inapotengeneza wazo la kukomboa maisha yako jua hapo hauko peke yako,  namaanisha akili yako inaposhtuka na shetani anashtuka na kuangalia upande wako. Haswa kwenye mambo ambayo unakuta tunayapenda tukishayapatia wazo zuri  shetani huanza kuangakia njama za kuvunja upendo ndani ya moyo wako,kwa lugha nyepesi huanza kuweka mbegu ya chuki au mbegu ya husda na hapo unakuta mtu anapoteza muda kuanza jambo lako lakini kumbe kupoteza muda ule ilikuwa ni kama kulima,kupanda na kupalilia chuki kweye wazo lako mfano mzuri angalia wewe mwenyewe mawazo mangapi katika maisha yako yamekuja na muda ulivyozidi kwenda na wewe unashangaa hamasa ya kulitenda inaisha na mwisho wa siku unaacha kabisa kulifanya?  Hata mimi huwa inanitokea na nilijifunza, leo hii hali kama hii hunikuta nikiwa nishaanza kuchukua hatua katika mambo yangu na hata kama nafsi hii ikianza ushawishi wa kuweka mbegu hiyo huwa najipa moyo na kusali pia. Nakumbuka nilivyokuwa naandika kitabu cha AKILI YA USHINDI ilikuwa inafika kipindi naona bora niache lakini nilikuwa nikisimama na kuombea kitabu niweze kukimaliza na hatimaye Mungu alisaidia kikamalizika.

Hebu leo usikubali kuacha nafasi ya kuanza jambo lako kwa shetani afanye yake,usijipe moyo tu alafu ukasema kesho nitafanya hivi,anza leo kama ni biashara toka anza kuifanya bila kujali unakiwango gani cha hela wala usiangalie wewe kuwa msomi kwahiyo lazima uchague kazi,sikiliza usiruhusu cheo au title yoyote kukuchagulia kazi ila acha akili na moyo wako vikwambie flani you belong there na kweli nenda kwa moyo wako wote hata kama unahela ndogo.Tuangalie wengi waliotumia title au vyeo vyao kuchagua biashara leo hii wamefika wapi? wengi wameweza kufika sehemu flani kwa kufanya walichokichagua lakini wamepata nusu ya matokeo kama wangeamua kutumia Akili na Mioyo yao kufanya mambo ambayo wanayapenda.

Kujifunza zaidi unawea kudownload Applications ya LAZAROSAMWEL  kwa kuclick link hii kwa chini ⬇⬇⬇⬇
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.lazarosamwel.app

Ulikuwa nami;

Lazaro Samwel 
Life Coach 
0753616584/0653386586
Blog;www.lazarosamwel.com
Email;akiliyaushindi17@gmail.com au lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment