"Ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii" na "Ukimwelimisha mwanamke umemkomboa mwanaume" sijui wengine wanachukuliaje swala hili ila kwa mawazo yangu kwa ufupi, licha ya mwanaume kuitwa kichwa katika familia bado mwanaume anatakiwa kutenga muda kumjenga mke wake kuhakikisha anakuwa na maarifa na kujitambua zaidi.Mwanaume ni kichwa katika familia kwa kufungua ujinga wa mke wake akitambua akiuacha ujinga huo shetani atautumia kumwangamiza yeye mwenyewe.Ndio maana wazee wetu wanasema "mwanamke anahatma kubwa sana katika maisha ya mwanaume" Shetani ni mjinga lakini ni mwerevu kwa kuchagua watu wenye spana za kulegegeza nati watu waliozikaza kwake. Mfano mwanaume ambaye anampenda sana mke wake na huwa anamsikiliza na kumpa nafasi katika maamuzi, kama mwanaume atashindwa kujijenga na kumjenga mke wako katika imani ya kweli kuamini katika Mungu atakuwa anatengeneza lango la shetani kumharibu kupitia mke wako.
Bila ubishi mwanamke ana ushawishi mkubwa sana ukibisha angalia Adam kama angekuwepo ningekwambia umuulize ilikuwaje akakubali kula Tunda la mti wa mema na mabaya wakati alikuwa anajua kabisa alishakatazwa kufanya hivyi, soma habari za Samsoni angakuwepo ningekwambia umuulize nini haswa kilimfanya atoe siri ya nguvu zake kwa Delila mpaka kuondolewa macho au kilimfanya nini kumpenda yule dada wa Gaza ikiwa anajua kule kuna maadui zao? soma kidogo habari za Daudi nini haswa alivutiwa kwa Bathsheba? Hii ni baadhi mifano kwamba mwanamke akielimishwa pia bado kuna mambo ambayo sisi wanaume hatuwezi kuyakwepa tunaweza kuyakwepa. Lakini mwanaume unaweza kupuuzia kumjenga mke wako na akawa mharibumkubwa katika jamii kupitia shetani, kuna mambo utaanza kusikia , mke wa flani anatabia flani na flani au mke wa flani yuko hivi. "Your Wife is Your reflection" tutumie ukichwa wetu katika familia zetu kujijenga wenyewe kupitia wake zetu.
Lazaro Samwel
Life Coach
0653386586/0753616584
Email; lazarosamweli41@gmail.com au akiliyaushindi17@gmail.com
0 comments:
Post a Comment