Unabiashara lakini inawezekana hujui jinsi ya kupata wateja,mimi na wewe tunamajibu ya vitu gani tunaweza kuvitumia kuwavuta wateja katika biashara zetu.Leo hii jaribu kukaa tafakari ni vitu gani 10 ambayo huwa vinakushawishi kwenda kwenye biashara za watu wengine orodhesha katika karatasi japo vinaweza kuwa zaidi ya idadi hiyo alafu angalia kwenye biashara yako kimekosekana kitu gani? vitu ambavyo vinakuvutia kwenye biashara za wengine vinaweza kukupa somo nini unatakiwa kuboresha katika yako.Kama wewe kwenye biashara ya mtu flani kinachokuvutia ni maongezi ambayo huwa mnafanya inabidi na wewe utafute namna ya kuboresha jinsi ya kuzungumza na wateja wako,kama wewe unavutiwa kwa usafi katika biashara ya mtu flani huna budi na wewe kuangalia namna ya kuboresha kuwavutia wateja wako,kama ni ubora wa bidhaa huna budi kuangalia namna ya kuboresha ubora wa bidhaa zako. Usivichukulie kawaida kama wewe ni mfanyabiashara na ukaona suluhisho lake katika biashara ingine.Kubali kuwa makini na kujifunza zaidi.
Ulikuwa nami;
Lazaro Samwel
Life Coach
0753616584/0653386584
Blog: www.lazaroamwel.com
Email:akiliyaushindi17@gmail.com au lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:
Post a Comment