Wednesday, August 30, 2017

JITAFUTE USITAFUTE WENGINE


#Akili Ya Ushindi Talk🔝

Tafuta sauti yako,tafuta tabia yako halisi inayokubeba wewe uonekane wewe,kuwa wewe usiangalie mwingine kukuingilia jinsi ulivyo wewe kuwa yeye.Usishawishike na mtu yoyote ili umridhishe yeye na wewe upoteze hadhi ya kuitwa flani kama ulivyo.

Nikwambie siri moja Katika maisha yako ukiona akili yako inawaza kuwa mtu flani jua unapotea na hauwezi kufanikiwa kuwa wewe.Usitumie mapungufu uliyokuwa nayo leo ujiache mwenyewe na utamani kuwa mwingine.Acha mapungufu katika changamoto zako cha msingi usiwe mvivu kujifunza kwenye mapungufu yako na kuchukua hatua kwenye mafunzo hayo ukiwa ndani ya himaya yako.

Unapojaribu kuwa mwingine na watu wanajua unatakiwa kuwa kama ulivyo kwanza unapoteza uaminifu wao kwako mfano mzuri haujawahi kumsikiliza mtu flani anajitahidi kuwa na sauti kama ya mtu flani alafu wewe unapata aibu ya kumsikiliza kwasababu unajua hiyo sauti sio yake ni ya mtu flani?  wengine huwa mpaka wanajificha kumsikiliza mtu huyo.Au unaambiwa kuhusu mtu flani ambaye anaweza kuwa rafiki yako jinsi anavyoigiza kuwa mtu flani ghafla wewe unajisikia aibu kwasababu unajua sivyo alivyo.Utakuwa unapoteza uaminifu kwa watu kwako.

Ulikuwa nami;
Lazaro Samwel
Life Coach
0753616584/0653386584
Blog: www.lazaroamwel.com
Email:akiliyaushindi17@gmail.com au lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment