Thursday, August 31, 2017

MAMBO 5 KIJANA UNATAKIWA KUYATAMBUA KUSONGA MBELE.


"Huwezi kuongeza usichokuwa nacho na huwezi kupunguza usichokuwa nacho. Hauwezi kulalamika kutokusonga mbele ukiwa huna hata cha kusonga nacho mbele".- Lazaro Samwel

1. Usidharau mawazo unayozalisha katika akili yako.

Vijana wengi kwa sasahivi tumekuwa hatuna nidhamu ya mawazo ambayo tunazalisha katika akili zetu ndio maana asilimia kubwa tunaenda sehemu moja ya kutaka kuajiriwa na sio kujiajiri.Kila wazo unalozalisha liandike na lipe tathmini katika maisha yako.jiamini.

2. Usitake kila kitu unachokifanya ulipwe.

Haswa tunapoanza kujenga misingi mizuri ya maisha yetu mfano unatafuta ajira usikimbilie kwanza kulipwa  lakini jitoe kufanya kazi kwa juhudi na kwa umakini kuonesha utofauti wako ikiwezekana fanya kazi kama tayari unalipwa katika sehemu uliyojitolea. Omba kujitolea kwanza kabla ya ajira maana nafasi za ajira ni chache .

3. Kijana kubali kujifunza.

Janga kubwa la watanzania haswa lipo kwenye kujifunza hili ni swala gumu haswa kwa vijana na ndio maana wengi huona kwa macho kila kitu kimeshafanywa ikiwa kuna watu wanaona kwa akili kuna mambo bado hayajafanywa kwa usahihi. Kuna kijana ukimwambia kuhusu kusoma vitabu anaona kama unamchangaya akili lakini kusoma vitabu inatakiwa kuwa na ulazima wa kijana kufanya hivyo. Kuna mwingine akipata ajira ndo kabiaa anaona haina haja ya kusoma vitabu au kujifunza mwingine amemaliza chuo na anahangaika na ajira anaona hakuna umuhimu wa kusoma vitabu saaa ni fursa gani ambayo utaipata na isihitaji maarifa? Hakuna.Hata kwa watu ambao wamefanikiwa jifunze pia mfano mimi huwa najifunza na kuchukua hatua mambo ambayo  watu wengi waliofanikiwa husisitiza kwa asilimia kubwa na hata mambo mapya ambayo huwa wanasisitiza,unawwza usinielewa nachomaanisha kama kila mmoja anakazia kujifunza kwa kusoma vitabu lazima hapo kuwe na kitu.

4. Kuwa na uvumilivu.

Sisi vijana uvumilivu ni kila kitu na sio kuwa na haraka ya kutaka leo ufanikiwe wakati hata misingi bora hatujaweka.Kitu ambacho tunakosa ni uvumilivu yani tunataka kuamka matajiri ikiwa leo tumeweka mipango.Nikupe siri moja,tunaposema uvumilivu ni kuwa na subira huku ukiwa unajifunza kwa makosa unayoyafanya katika jambo lako lotote ambalo umeanza kulifanya,huko kutakusaidia kupata unachokitaka.

5.Usidharau kitu ambacho unauwezo nacho au mtu flani anauwezo nacho.

Usiwe mbinafsi unaweza kuwa na 1 lakini unahitaji mbili na ukaangalia kwa pembeni kuna mwenzako ana 1 lakini hajui kwamba anamoja usiwe mbinafsi mshirikishe kwani unataka mbili na muungane kufaidika na 2 kwapamoja.Hii moja inaweza kuwa wazo la biashara lakini mwenzako ana moja ingine kufanya lile wazo lifanyiwe kazi,unganeni pamoja mfanye kitu.


Ulikuwa nami;

Lazaro Samwel
Life Coach
0753616584/065338654
Blog;www.lazarosamwel.com
Email;akiliyaushindi17@gmail.com

0 comments:

Post a Comment