Friday, September 1, 2017

KIJANA MZALENDO NA TAIFA LAKE.


Wiki hii baada ya kupitia habari nyingi katika vyombo vya habari iliyokuwa gumzo ni ya watu/vijana 56,000  walikuwa wakifanya interview kutokana na nafasi 400 za kazi kutangazwa.Ukiangalia kiundani zaidi ni kwamba kwenye  watu 140 ambao walikuwa wanafanyiwa interview ni 1 tu ndiye aliyekuwa anatakiwa kuchaguliwa na wengine 139 kurudi makwao kuendelea na maisha,na kama wengine walikuwa tayari wamejiajiri sehemu watarudi pia. Lakini kwanini haya yote yanatokea? Kuna kitu kinahitaji kubadilika haswa kwa sisi vijana kwa kujiamini sisi wewe na kupeleka uoga wa kumtumikia mtu mwingine kwasababu vijana wengi tunajiogopa na kuweka imani kwa watu wengine kiasi kwamba hata tunapopata mawazo mazuri tunayapuuzia tunaona mpaka tupewe kazo ndipo tunaweza fanikiwa.Kwa upande wa Serikali inatakiwa kuonesha vipao mbele katika sector zingine na sio elimu ya darasani tuu. Kama tunaweza kutenga bajeti kwaajili ya ujenzi wa barabara au kuweka mikakati ya kulinda wanyama pori basi hata serikali inaweza kujenga vituo vya kukuza watu katika sehemu wanazozipenda. Vijana wengi wakitanzania wanajua wanachotakiwa kukifanya na wanajua wapi wanaweza kutoka kimaisha lakini ujasiri wa kufuata ndoto zao ni mdogo kwasababu ya kufuata hamasa ya kijamii kwamba ajira ndiyo itakutoa kimaisha,hatukatai kwamba kuna watu wanafanikiwa japo sio sana katika ajira lakini sio kila mmoja ameumbwa na kuwekewa karama ya kuajiriwa. Ukitaka kuthibitisha hili angalia vijana wangapi wakitanzania wanasoma kitu flani mwisho wa siku wanaishia kufanya kitu kingine? Angalia vijana wangapi wa kitanzania wanaona ni bora nimalize chuo tu nipate cheti?  Angalia vijana wangapi wakitanzania wanasomea kuvaa joho la chuo na sio joho la kukomboa fikra zao na jamii zao pia? Bado napata maswali kwamba elimu inahitaji hela au inahitaji kutoa vijana walioiva kuwa chapa ya taifa yenye kuongeza thamani zaid ya hela?  Bado najiuliza katika wale watu 56,000  serikali ikikaa kiumakini na kuweza kuwapa interview nzuri tungepata wakina steve jobs,Aliko Dangote, Mo Dewij,  Nelson Mandela, Mwl. Nyerere, Nkwame Khuruma, Shakespeare, Shabani Robart,Galilei Galileo,Thomas Sankara, Plo Lumumba wangapi?  Bado najiuliza kwelii serikali inaweza kuridhika na 55,600 kurudi nyumbani na kujisifu wanawasomi wengi ikiwa maendeleo hayaendani na idado ya wasomi tuliokuwa nao mitaani wenye uwezo wa kupunguza mapungufu ya taifa letu? Itakuwa bado haina maana ya kuwaacha mpaka wamemaliza masomo yao.

Inabidi Tanzania tuache utani haswa katika sekta ya elimu serikali iangalie swala hili kwa ikaribu.Sawa ajira zinaweza zisitoshe kila mmoja lakini give support kwa vijana katika sekta tofauti na isiwe kwa maneno ya kisiasa ili waweze kuamini katika kiu waliyokuwa nayo ndani yao. Napenda kupongeza mashirika binafsi na baadhi ya kiserikali kwa kujiweka kipao mbele kuiamsha serikali kutambua kwamba vijana wanavitu vikubwa sana ndani yao. Kauli ya Mh raisi ya kwamba wanahitaji serikali ya viwanda haiwezi kutimia bila kuwapa vijana nguvu katika mambo ambayo wanayafanya. Na kijana kutokufika chuo isiwe kikwazo cha kuambiwa kwamba hawezi kupata ajira ni vyema kuangalia kwa ukaribu  uwezo wa mtu kuliko cheti cha mtu na alama zake. Nilishawahi kuandika kwa kuuliza watu Albert Einstein alipata division ngapi au alikuwa na elimu gani ya darasani?  Plato alipata alama ngapi kwa kipindi chao?  Socrates alikuwa na kiwango gani cha elimu kwa kipindi kile? Daudi, Mfalme Sulemani na vitabu vyake vya busara alikuwa na elimu gani zaidi ya hekima na busara?  n. k hawa wote hata  kama utasema kwamba kipindi kile na hiki ni tofauti lakini walifanya makubwa kwa kufanya vitu walivyovipenda na hawakuwa wamefungwa kufanya mambo yao licha ya changamoto walizokumbana nazo. Ni sawa na sisi vijana tukipewa uhuru wenye mfumo mzuri wa kusaidi mambo mazuri vijana wanayopenda kufanya Tanzania ya viwanda itafika mbala sana na tunaweze punguza haya mambo ya watu 56,000 kupigania nafasi za kazi 400.

Kama bado hujajiunga na program mpya ya AKILI YA USHINDI tembelea www.akiliyaushindi.com kuwezajujisajili katika program hii ili niweze kuwa pamoja nawe kwa mwaka 1 kukuongoza katika shughuli unayoifanya. 

Hizi ni salamu zangu kwako.


Ulikuwa nami;

Lazaro Samwel
Life Coach
0753616584/0653386586
Email; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment