Bila ubishi mwanamke ana ushawishi mkubwa sana ukibisha angalia Adam kama angekuwepo ningekwambia umuulize ilikuwaje akakubali kula Tunda la mti wa mema na mabaya wakati alikuwa anajua kabisa alishakatazwa kufanya hivyi, soma habari za Samsoni angakuwepo ningekwambia umuulize nini haswa kilimfanya atoe siri ya nguvu zake kwa Delila mpaka kuondolewa macho au kilimfanya nini kumpenda yule dada wa Gaza ikiwa anajua kule kuna maadui zao? soma kidogo habari za Daudi nini haswa alivutiwa kwa Bathsheba? Hii ni baadhi mifano kwamba mwanamke akielimishwa pia bado kuna mambo ambayo sisi wanaume hatuwezi kuyakwepa tunaweza kuyakwepa. Lakini mwanaume unaweza kupuuzia kumjenga mke wako na akawa mharibumkubwa katika jamii kupitia shetani, kuna mambo utaanza kusikia , mke wa flani anatabia flani na flani au mke wa flani yuko hivi. "Your Wife is Your reflection failure" tutumie ukichwa wetu katika familia zetu kujijenga wenyewe kupitia wake zetu.
Lazaro Samwel
Life Coach
Email; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment