Wednesday, August 16, 2017

Positive Mind Vibe Quotes

🔰Kusema unajiheshimu sio kuheshimu ulivyokuwa navyo tuu lakini pia kuheshimu vya wengine ni kujiheshimu. Heshima haitawezs kujengwa kwa kudharau mtu kwasababu hayuko nafasi uliyopo lakini unapoheshimu nafasi ya kila mmoja ni sehemu kubwa sana ya kujenga heshima yako.

🔰Wanauchumi wanasema hauwezi kuzalisha kisichotumika. Na wanafalsafa wanasema hauwezi kupokea usichotoa mfano kwa mfanyabiashara usitegemee kupata matokeo mazuri katika biashara yako kama unatoa huduma mbovu na hauwezi kupata manufaa mazuri kwa kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya chini kwa wateja wako maana unachokitoa ndicho utakachokipokea.


🔰Unataka furaha katika maisha jiulize wewe unaowadai kukufurahisha umewafurahisha je? Jiulize wale ambao unataka msaada wao wewe umewasaidiaje? Na kama umesaidiwa na ukawa katika hali flani nzuri unatumiaje hali yako nzuri kusaidia wengine?
Usipojifunza kwa kupokea kwa aliyekupeza hauwezi kujua kuwapa wasiopezwa.

🔰Unachokidharau kutokuwa na dhamani unakiongezea thamani  na unayemdharau kwa udogo wake unamwongezea nguvu kwa kudogoza ukubwa wako.


Lazaro Samwel
Life Coach

0753616584/0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment