Friday, August 18, 2017

MAMBO 3 MUHIMU KUYAJUA


 
Karibu mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel nikiamini kiu yako kubwa ni kutaka kuona unafikia malengo yako.Inawezekana imekuwa ni safari ndefu sana katika maisha yako kuhakikisha kwamba picha iliyoko katika akili yako inaweza kutimia na kuwa katika hali ya uhalisia jinsi unavyotaka kuwa. Leo hii ningependa kukushirikisha mambo makuu matatu ambayo kama utaweza kuyafuata katika maisha yako yako lazima ufika sehemu nzuri.Vitu hivi inawezekana vikawa ni vigeni au ukawa ushawahi kuvisikia katika harakati zako za kila siku,lakini hauwezi kutoka mtupu kwenye somo hili;

1. Lazima Ujue umuhimu wa muda.
Muda katika maisha ya binadamu ni muhimu haswa katika kuhakikisha kwamba mambo yake yanatimia,ukiangalia katika kuweka malengo  yako kuweza kutimia muda lazima uzingatiwe. Ukiachana na malengo yako muda usipoweza kuutambua nao hauwezi kukutanbua katika kuhakikisha unajenga misingi mizuri kwa kizazi chako na familia yako kwasababu maono yako uliyoyawekea malengo yanaweza kutimia kwa kuhakikisha kwamba muda unatumika ipasavyo.Kama ulipanga utafanya kitu flani kwa muda flani kweli unatakiwa kuhakikisha unatendea haki muda wako.

2. Jitahidi kusaka elimu kuhusu kitu unachopenda ufanikiwe.
Ukishajua kitu ambacho unataka ufanikiwe katika maisha yako haina maana ni mwisho wa kusaka maarifa ila ndio mwanzo kabisa wa kuzidi kuongeza maarifa ili usonge mbele zaidi ya hapo ulipo. Hata umuhimu wa muda utaujua kwa kuwa na maarifa kupitia elimu uliyokuwa nayo.

3. Jua unapotaka kufika katika maisha yako.  Unapojua umuhimu wa muda na ukawa na maarifa ni lazima pia ujue unapoelekea.Kujua unapoelekea kwanza inakupa hamasa ya kusonga mbele zaidi hii inakusaidia kutokukata tamaa au kuwa kigeugeu katika kusikiliza kila unachoambwa.


Lazaro Samwel
A Life Coach Coach
0753616584 / 0653386586

Email;lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment