Inawezekana na wewe ukawa ni muhanga wa swala ambalo naenda kuliezea leo lakini leo unaenda kupata suluhisho.
Umeshawahi kutumia sentensi hii kutafuta wazo la biashara?
"Nina laki 2,3,4,5 au milioni moja naweza kufanya biashara gani?" kama umeshawahi kutumia sentensi kutafuta fursa au wazo la biashara ya kufanya unafanya makosa na unapishana na biashara nyingi na nzuri ambazo zingeweza kukufanya ufanikiwe katika maisha yako. Nakwambia hivi kwasababu ukiweka kiwango cha hela mbele kutafuta wazo la biashara kwanza unajiweka katika sehemu kubwa ya kufanya fursa ambayo sio sahihi katika maisha yako mfano ukasema unataka wazo la biashara la laki 5 itakuaje ukikutana na biashara yenye kukuhitaji laki 9? Lazima utaiacha kwasababu kwa kiwango ulichojiwekea umejifunga tayari, lakini kumbe kiwango kikubwa cha pesa haimaanishi hauwezi kuanza kuifanya na ukafanikiwa.Unachotakiwa kukifanya ni angalia wazo bora la biashara bila kujiwekea mipaka ya hela uliyokuwa nayo alafu ukishalipata wazo hilo ndipo uangalie kiwango cha hela ulichokuwa nacho unawezaje kuivunjavunja ukaanza kwa udogo lakini malengo yako yakawa kukufikisha kule pakubwa ambako mwanzo haukuweza kuanza nako.
Unaweza ukawa unajiuliza kwamba unawezaje kupata wazo la biashara? Njia rahisi anza na biashara ambazo unaziona pale unapoishi na maeneo mengine ambayo pia huishi mana biashara unaweza kuiamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu ingine mfano Upo Mwanza na unaona sehemu ambayo unaishi hakuna mgahawa lakini kwa Dar es Salaam umevutiwa na mgahawa flani ambao ulishawahi kwenda kupata huduma pale,utachofanya ni kuhamisha ulichokiona Dar es Salaam na kukileta mwanza. Kwa maeneo ambayo unaishi unaweza kukaa chini na kuorodhesha fursa zilizopo na mapungufu yake na ukaangalia ipi yenye mapungufu mengi na wewe ukaangalia jinsi ya kurekebisha kupitia biashara yako.
Kuna mengi sana ya kujifunza lakini napenda kukushauri ewe mjasiriamali,uliyeajiriwa na ambaye hujaajiriwa usikose kitabu changu cha AKILI YA USHINDI kitakachotoka mwezi wa 9 kuweza kufunguka katika nyanja mbalimbali ulizofungwa kwenye biashara yako au ajira yako na katika maisha yako kwa ujumla.
Ulikuwa nami;
Lazaro Samwel
A Life Coach
0753616584/0653386586
Email; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment