"Usifanye kitu uonekane unakifanya fanya kitu kionekana kinafanywa na wewe" - Lazaro Samwel
Nikupe siri moja kwamba sio kila mwenye mawazo hasi hana mawazo chanya, kunawatu wenye mawazo chanya lakini kwa lengo la kufanya wengine kuwa na mawazo hasi au kuwa kama yeye, haujawahi kukutana na mtu ambaye ukikutana nae kwa siku ya kwanza unaongea nao mambo chanya tena vizuri sana na anaweka pointi ambazo zimenyoka kwelii lakini mnavyozidi kujenga na uhusiano anaanza sasa kukuingiza kwenye uhalisia wake wa hasi? hawa naweza kuwaita Pareto Mindset yani wao wako hivi 20% ya akili zao ni chanya na wanazitumia vizuri kweli kuficha 80% ya akili zao ambazo ni hasi, hawahawa ukikaa nao muda mrefu kama nilivyokueleza 80% ya akili hasi ambazo ndo uhalisia wao huanza kutafuta watu wenye 80% ya mawazo chanya na 20% mawazo hasi kuweza kuwa 20% mawazo chanya na 80% hasi. Nimeshakutana na watu wa namna hii wao mara nyingi huwa kama wajuaji sana na huwa na mtindo wa kutaka kuonekana wako sahihi katika kila jambo,mara nyingi huwa wanatafuta ushahidi mambo yao ambayo hasi kuwa kwelii. Ukikuta kama ni kwenye magroup ya whatsapp wanaweza kuona kitu flani kiko sahihi lakini kwakuwa na chuki, wivu ataanza kutafuta njia ya kuweza kuangalia wangapi watamuunga mkono hisia zake na sio fikra zake kupinga swala au jambo ambalo liko kwenye group mana hapo tayari kashatawaliwa na hisia kutokana na mawazo yake hasi ya 80%, utaanza kuona na wengine wenye tabia kama yake wanajitokeza kuunga mkono au wengine ambao watashindwa na wao kufikiri wanajikuta wanaingia kwenye PARETO MINDSET. Hata katika maisha yetu ya kawaida tunakutana na hawa ndugu ambao wako na muundo huu.
Mambo haya madogomadogo ndiyo ambayo yanafanya tusisonge mbele, yanafanya tulalamike kila kukicha mambo hayabadiliki.Kutumia ubaya wako kuangusha wengine ni kitu kibaya sana na ni dhambi mbaya sana kwasababu unajua huyo ambaye unataka awe na mawazo hasi angeweza kusaidia wangapi kama angakuwa na mawazo chanya? au unajua ni wangapi kupitia huyo unayempotosha wangeweza kufanikiwa? je kama unayempotosha kwa mawazo hasi ndiye angekuwa mwokoaji wa familia yake na sasa familia yake imebaki kwenye mahangaiko kwasababu wewe umempotosha? vipi kama unayempotosha alikuwa anatakiwa kuja kuwa muelimishaji mzuri katika jamii na wewe ukampandikiza 80% ya mawazo yako hasi? Unadhani lawana za hawa watu ambao watakuwa wanalalamika kukosa mkombozi wao zitakuwa zinakuja kwa nani? mwisho wa siku utaanza kusema unalogwa, hapana , acha kujiloga.
Hauwezi kupata wazalendo wazuri wa nchi bila watu kuwa wazalendo wenyewe kwenye Akili na miili yao.Hauwezi kuwa na siasa safi kama watu hawana siasa safi za maisha yao. Lakini kumbuka uzalendo wako bora na siasa yako bora ya maisha haiwezi kujengengeka bila kuwa na FIKRA CHANYA, hata inchi yako haiwezi kukuita mzalendo ukiwa na mawazo hasi.
Kuwa makini.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386586
Email : lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment