Tuesday, July 4, 2017

SWALI MOJA MUHIMU KULIJUA KUHUSU BIASHARA YAKO

Image result for pure mindset in business
Kuna swali 1 ambalo leo ningependa kukushirikisha na inawezekana wewe ukawa ni mmoja wa wahanga wa swali hali kwenye biashara yako.Swali hali linalenga kuhusu biashara mana nauhakika asilimia 98% ya watu duniani wanajihusisha na biashara na naimani unanielewa navyosema kufanya biashara sio lazima ufungue duka au sio lazima uwe na frame uwe unafanya biashara, hata yule ambaye anaimba anafanya biashara, yule anatoa ushauri anafanya biashara, yule anatumia nguvu kufanya kazi na akalipwa anafanya biashara pia.  Haya maswali mi maswali gani? 

1. Kwanini biashara yangu haikui?

Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa makala zangu na kama utakuwa umesoma kitabu changu cha NGUZO 3 ZA MAISHA nimeongelea sana kuhusu kubadili fikra, haswa kwa wewe mfanyabiashara ni LAZIMA na SIO OMBU ubadilishe mtizamo wako kama unataka biashara yako ikue. Haswa biashara yako kutokukuwa ni kwasababu bado unaiona biashara yako kama unavyoiona kipindi hichi, kama unamiliki duka na unaona duka lako halipanuki ni kwasababu bado unaona duka lako kama unavyoliona sasahivi. Ondoa hiyo mitazamo ya sasahivi na wazia biashara yako kwa ukubwa zaidi. 

Lakini jambo lingine muhimu zaidi baada ya kubadili fikra zako lazima pia ujue jinsi ya kutumia mapato yako na kuangalia jinsi gani unaweza kuweka hela na ikazalisha zaidi kwa kupanuka kwa biashara yako.Wewe umeanza biashara faida ya kwanza umepata 200,000/= unajitoa out kwenye hotel moja nzuri tuu Dar au Mwanza, ndugu kwa tabia hii usitegemee kukuza biashara yako kama hutaweza kubadilika. *Faida ya mwanzo ambayo unaipata kwenye biashara yako ni kwaajili ya kukuza biashara yako na sio kukuza mwili wako*. Kwa upande mwingine naweza kukupa mfano kama unanunua nyanya tenga 1 kwa 40,000/= katika lile tenga ukapata faida 20,000/= inamaana tenga zima linakupa 60,000/= na ukitoa 40,000/= ya kununua tenga la nyanya ndipo tunapata ile faida ya 20,000/= ( hapo sasa tufanye kutoa gharama za kusafirisha kuja kwako n.k ni 5000/=) kwahiyo unabakiwa na 15,000/= hii faida usiitumie kwa matumizi yako binafsi jitahidi kuweka akiba hata 10,000/=, na kama tenga la nyanya linaisha baafa ya siku 4 inamaana baada ya siku 16 kwa kuweka akiba ya 10,000/= utakuwa umetengeneza 40,000/= na utaongeza tenga lingine la 2 la 40,000/= na biashara yako hapo sasa itakuwa inaanza kukua mana kutoka kwenye tenga moja kwenda 2 ni hatua nzuri. Chukua huu mfano hata kwenye biashara zako zingine kila bidhaa unayoiuza hakikisha unajua faida yake inawezaje kuongeza bidhaa ingine ya 2 kupitia faida yake?

USILE FAIDA kwa kukuza mwili wako lakini tumia faida yako kukuza biashara yako. Simaanishi ukaacha mwili hovyo hapana mfano wa hapo kwenye nyanya nimekuonesha jinsi ya kutenga kiwango flani cha pesa kwaajili ya kuhakikisha na mwili unapata kitu kuqa na nguvu.

Lazaro Samwel 
Young Life Coach 

0753616584 / 0653386586

0 comments:

Post a Comment