
Haujakosa biashara ya kuanza kufanya ila kunamambo ambayo unatakiwa kuyatambua katika akili yako na kuanza kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo. Ila ningependa kukwambia kwamba wewe mpaka hapo ulipo ni BIASHARA tosha na bado ni MAFANIKIO ambayo unayahitaji. Unaweza ukawa uko njia panda na haujui kwamba utapata wapi wazo la biashara na ukadhani kwamba ni lazima uwe na mpango biashara kwanza. Mpango biashara ni Muhimu lakini lazima uangalie na karne hii inapoelekea ni karne ambayo inaenda na spidi lakini kwa umakini mkubwa wa kuelewa unachokifanya. Wazo lako la biashara haliwezi kuwa nje na akili na mwili wako kabla ya kuanza kuangalia mazingira yako ambayo unaishi. Leo nataka nikufungue na nikupe akili ya ushindi ewe kijana ambaye kila siku unawaza jinsi ya kujikwamua kimaisha kupitia biashara na inawezekana unawazo lakini hujui pa kuanzia. Unajua sababu kubwa ya kutokuanza biashara ni nini??
Sababu kubwa ya watu kutokuanza biashara ni kwasababu unadhani kwamba biashara ni lazima uwe na hela ya kuanzia, hapana, ngoja leo nikupe akili ya ushindi kwamba inachukua 0 kufika 1 lakini itakuchukua 1 kufika 2 na moja kufika 3 na kuendelea. Ni sawa na wewe kila siku kuwaza kuhusu mtaji, kama utakuwa makini mtaji 0 ni akili na mwili wako kukupeleka kwenye biashara ambayo unataka kuiendeleza zaidi.MTAJI PESA ni muhimu kukusaidia kukuza biashara yako na sio kuanza biashara yako. Naomba hapo unielewe kwamba itakuhitaji akili na mwili wako kubadilisha mawazo yako na kuwa biashara. Mfano unaweza kuanza kuongea na kuelimisha watu ukalipwa lakini jua kuongea tuu tayari ni biashara, unaweza kutumia mikono yako kusaidia mtu kazi akakulipa tayari hiyo umefanya biashara, wewe ni mwanafunzi wa chuo ambaye umemaliza mwaka huu tena ulikuwa ukisoma kiswahili na uko vizuri unaweza kutumia ujuzi wako katika kuhakiki kazi za waandishi hiyo nayo tayari ni biashara, wewe kuwa mtaani na kuwa na ujuzi wa kutengeneza vifaaa vya umeme hiyo ni biashara tayari, unaweza kuomba kufanya kwa watu na hiyo kazi ikakupatia hela ya kuendeleza biashara yako.
Nachomaanisha ni kwamba vijana inabidi tubadilishe fikra na kuanza kujiangalia wenyewe ni lazima tujitahidi kujitembelea wenyewe ndani yetu na kuweza kuangalia vitu ambavyo tunaweza kuanza kuvifanya na baadae kuweza kuviendeleza zaidi. Wengi tunawaza pesa kwanza katika kila jambo na muda unaenda hata mawazo ambayo tulikuwa nayo yanapotea na hayazai chohote.
Ni Muda wa kuwa na AKILI YA USHINDI sasa.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment