"Unaruhusiwa kuanza biashara yako kwa udogo lakini usiruhusu kuwaza kwa udogo biashara yako.Ukiona hiyo hali inakujia ikemee kabisa iambie naona Kampuni, naona Umilionea ubilionea kupitia biashara yangu wacha niwaze kwa mapana zaidi ya udogo wangu wa mwazo " - Lazaro Samwel
Mafanikio yoyote katika maisha yako yanaanza kwa kuanza kidogokidogo kwa hatua ndogo lakini mawazo makubwa,kama ni biashara haijalishi umeanza na mtaji wa kiwango gani.Usiogope changamoto katika safari yako ya mafanikio.Kama kweli umeamua kuanza safari hiyo jua kwamba ishara mojawapo ya kujua kwamba umeanza ni utaona kufeli kwingi sana, kukatishwa tamaa kwingi sana,kutengwa na ndugu zako kutakuwa kwingi,kudharauliwa na kuonwa kama kichaa kwa mawazo makubwa ambayo unayo ukiwa bado katika safari yako ya mafanikio, muda mwingine inawezekana kwamba umestafu au unakaribia kustafu na watu wanakwambia umri umekwenda wewe subiri kufa tuu hauwezi kufanikiwa,amka sasa na hebu twende pamoja,
Colonel Sanders Mwanzilishi wa Kentacky Fried Chicken (KFC) Restaurant katika Umri wa miaka 5 alifiwa na baba yake,miaka 16 aliacha shule, miaka 17 alikuwa tayari ameshapoteza kazi 4, miaka 18 aliamua kuoa, umri wa miaka 20 mke wake alimuacha na kuchukua watoto. Akaamua kuwa mpishi katika Mgahawa mkoja mdogo lakini bado akawa anamlazimisha mke wake kurudi japo ilishindikana. Katika Umri wa miaka 65 akastafu kazi na akapewa na serikali cheki ya $105 kwanza alikata tamaa na akaona yeye kama ameshindwa maisha.Colonel Sander kwa kukata tamaa akafikia maamuzi ya kujiua kwahiyo akaketi kwanza kuweza kuandika wosia lakini cha ajabu badala ya kuandika wosia akaandika kile ambacho anataka kukikamilisha katika maisha yake na akawaza jinsi ilivyo mpishi mzuri, kumbuka Colonel Sander alikuwa na umri wa miaka 65. Ikabidi akope $87 kwaajili ya kuanza kufanya biashara yake na hapa ndipo KFC ilipoanza na kwa maajabu ya Mungu pamoja na juhudi zake alipotimiza miaka 88 aliweza kuwa Bilionea. Akasema "Niliweza kupata NDIO 1 baafa ya kupata HAPANA 1009 ". Subira,uvumilivu, kujiamini na kuwa na tafsiri yake ya mafanikio bila kuangalia anaumri gani ni jambo ambalo limemfanya Colonel Sander kuwa Bilionea. Safari ya mafanikio ni safari yenye hatua na hizo hatua sio za kuwa na furaha muda wote kama nilivyoeleza mwanzo kunamambo mengi njiani lakini hivyo vyote ni ishara ya mafanikio kwako.Kama umeona safari yako ya mafanikio itaanza kaa kufanya biashara usiangalie udogo wa hela au mtaji wa hela uliokuwa nao kuanza biashara yako lakini chunga kutokuaa na ufinyu wa mawazo, ona biashara yako mbali zaidi, kama ulikuwa unauza nyanya jitahidi kujiona unashamba lako la nyanya,mbogambona pamoja na matunda tena ndani ya kampuni yako ambayo wewe ndiye utakuwa msambazaji kwa wafanyabiashara wengine wadogo. Ukianza kujenga haya mawazo na kuanza kufanya kazi kwa juhudi lazima kunasiku tutaongea kivingine.Cha msingi ridhika na ulichokuwa nacho au ulichoanza nacho lakini usiridhike kuwa hivyohivyo kila siku jitahidi kuwa na mabadiliko mazuri .Kumbuka kwa umri aliokuwa Calonel Sander hiyo pesa ilikuwa ni ndogo sana na ukizingatia alikuwa mzee wa miaka 65 kwahiyo alikuwa na mahitaji mengi haswa mambo ya chakula, mavazi na sehemu ya kulala pia. Lakini Colonel hakulalamika na kunakitu alikifanya licha ya udogo wa hela ambazo alipewa ( $105 na $87) na kubadilisha maisha yake,kwa sisi tungesema kwamba hiyo hela aliyokuwa nayo ni kwa matumizi ya nyumbani.
Biashara ni moja kati ya usafiri ambao unafanya watu wengi wafike safari yao ya mafanikio salama hivyo ni kitu muhimu sana katika kubadilisha maisha yetu. Kwa fundisho la Colonel Sander mafanikio haswa kibiashara hayachagui umri na maisha unayoishi ila wewe ndiye unayefanya chaguzi ufanikiwe au usifanikiwe. Jaribu kufikiri Colonel Sander angeangalia umri wake unadhani angafanikiwa katika maisha yake? je angeangalia na changamoto ambazo amepitia katika maisha yake toka akiwa na miaka 5 unadhani leo hii tungeweza kumwita Bilionea aliyefanya maajabu kwa umri mkubwa hivyo?
Nikuambie kitu mpenzi msomaji kwamba maisha yenye changamoto huleta maana halisi ya maisha, usihofie kuona umri wako unaenda mbio amua kuanza na tafuta maana ya mafanikio katika maisha yako, usiwazie kuhusu changamoto ambazo umepitia kipindi cha nyuma angalia nini unataka kitokee katika kesho yako. Lakini moja kubwa zaidi toka njee na waoneshe ulimwengu umezaliwa kuwa mashindi licha wao kuona umri wako umeenda.Kama Kijana ambaye unapenda vitu vizuri na maisha mazuri jiulize unafanya nini na unavisingizio vingapi kila siku unavyo kuweza kutengeneza maisha yako ili usije kuanza kujuta na kutaka kujiua kama Colonel Sander? Jiulize hela ambazo unazichezea leo tena kwa umri mdogo hivyo ungeamua kufanya kitu cha maana ungekuwa wapi leo hii?
Ukiona Mungu anakupendelea kila siku pumzi kuishi jua kunajambo zuri anataka aone wewe unayejishughulisha unalipata.
Jitahidi kupata kitabu chako cha NGUZO 3 ZA MAISHA kwa 10,000/= tuu.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0683539684
Email : lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment