Tuesday, July 4, 2017

BIASHARA HAIITAJI UJUAJI KUPITA KIASI

Image result for KNOWING EVERYTHING


Ushawahi kujiuliza kwanini biashara yako haukui? naimani kama jana ulifuatulia makala zangu kunakitu ambacho ulikipaya . Lakini leo nataka nikueleze kwa ufupi sababu zingine ambazo zinakusababisha wewe kutokukuza biashaa yako. 

1. KUJUA KILA JAMBO.

Kama kiongozi katika biashara yako na kujichukulia kama mjuaji wa kila jambo ni moja ya jambo ambalo linaweza kukusababisha biashara yako kutokukuwa kabisa.Wewe unataka kuwa mhasibu, unataka kuwa afisa masoko, unataka kuwa afisa ugavi na vingine vingi, na ukiulizwa kwanini unafanya hivyo unasema kwamba unabana uchumi, hiyo sio kubana ushumi ni kuuwa uchumi wa biashara yako.Ndio maana kunaho watu ambao wako kwaajili ya hizi kazi ambazo wewe unataka kuzifanya zote.Sijasema kwamba kama kiongozi wa biashara yako unatakiwa kuwa giza kujua hayo mambo, hapana,unatakiwa kuyajua lakini kumbuka wapo ambao wanafahamu zaidi. Haujawahi kujiuliza kwanini Mark Zukerberg hafanyi kazi zote za facebook? au umeshawahi kumuona ofisini kwake akifanya kila kitu? Haujawahi kujiuliza ni kwanini Mo Dewij hafanyi kila kitu katika moja ya kampuni yake ya MELT? au umeshawahi kumwona anasambaza maji Tanzania nzima? Haujawahi kujiuliza kwanini Bakhresa haendeshi malori yake ya Azam au kwanini asiuze Ice Cream mtaani? sio kwamba anashindwa lakini anajua kwamba kunawatu ambao ni mabingwa katika hizo sehemu, au umeshawahi kumwona Dangote akisambaza sumenti? au umeshawahi kumwona Yuko kwenye ofisi zake za viwanda vyote Afrika tena kwa wakati  mmoja? Hapana, lakini sio kwamba wana giza kwenye hayo mambo ambayo yanafanywa na wale ambao wamewaajiri,wanajua na wanaelewa kinachofanywa katika sehemu muhimu zaidi kwenye biashara zao. Ukijifanya mjuaji na mbahili kwenye vitu ambavyo haviitaji ubahili unaweza kushangaa kwamba unabaki mwenyewe kwenye biashafa yako. 

Ujuaji mwingi bila kiasi katika biashara yako unaweza kujifilisi mwenyewe bila kujua.

Lazaro Samwel 
0753616584 / 0653386586


0 comments:

Post a Comment