
Usiache maisha yako yatawaliwe na changamoto utaona changamoto ni shida, lakini maisha yako yakitawala changamoto utaona changamoto kama sehemu ya maisha ya kujifunza.
Biashara ni kitu kizuri sana kama watu wataweza kutambua ujanja wake upo kwenye akili tuu na sio pengine.Ukiwa na kiu ya kutengeneza bidhaa au kutoa huduma bora kwa mteja wako hii itakusaidia kupata suluhisho la hela ambazo unazitaka lakini ukiwa na kiu ya hela sana kuliko kuhakikikisha kwamba huduma au bidhaa yako inakuwa bora vyote unaweza kuvikosa.
Bidhaa inatakiwa kubeba suluhisho kwa mteja na sio mbegu ya chuki kwa mteja baada ya kutumia bidhaa au huduma yako.
Kuna watu ambao wanapenda kuwa na bidhaa nyingi bila ubora wakidhani watatajirika mapema lakini kumbe siri iko kwenye bidhaa bora yenye kiwango bora kwa watu flani ambao aliwalenga.Huko ndiko unaweza kuwa unavyotaka.Ukiwa na bidhaa nyingi kwanza kuna gharama ambazo zitaongezeka sana mfano gharama za kufanya matangazo kufikia idadi ya watu ambao watamaliza bidhaa zako ambazo hazina ubora. Nakwambia hivi kwa sababu bidhaa bora huongeza idadi ya watangazaji wa bidhaa yako bila hata kuwalipa na ukiwa na bidhaa bila ubora utaongeza idadi ya watangazaji wa bidhaa yako kwa kuwalipa bila kuwa na matokeo mazuri. Bidhaa bora haiwezi kumfunga mtu mdomo wake kuiongelea sehemu flani kwasababu automatical kila mmoja anataka ufahari wa ubora wa kitu flani hata kama sio chake, haujawahi kukutana na mtu unamwambia natafuta simu flani anaanza kukuelezea baadhi ya simu bora alizotumia tena na akakusisitiza kwenda kuichukua kwani unadhani kampuni ambayo anaipigia debe simu yao inamlipa hapana lakini kutokana na mtu kuridhika na ubora wa bidhaa na kutaka ufahari anafanya kwa kujitolea bila malipo yoyote lakini faida inakuja kwa wewe ambaye ulichukua muda wako kutengeneza bidhaa bora kwa kiwango bora zaidi.
Lakini pia tusisahau kwamba bidhaa ambazo hazina ubora zina mgharimu mtu kwa kuwa na umuhimu mdogo ndani yake na manufaa makubwa.Napozungumza kuhusu manufaa namaanisha kitu kuwa na kikomo cha haraka yani utakihitaji kwa muda mfupi sana tena pale tuu unapoona kuna uhitaji wake baada ya kukosa bidhaa ingine lakini tunaposema bidhaa kuwa na Umuhimu ni bidhaa kuhitajika na mtu kwa muda mkubwa zaidi,yani mtu asipokuwa na hiyo bidhaa bado haridhiki au kuwa na amani huo ndo umuhimu na kitu ambacho kitakusaidia katika biashara yako kama mfanyabiashara baada ya kutengeneza biashara yenye umuhimu kwa watu.
Kwa wale wahitaji wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA tunaweza wasiliana.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386585
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment