Kwenye maisha hauwezi kuanza kwa kufika sehemu ambayo unaitaka bila kuwa na vizingiti flani na sio lazima kila kitu ambacho unakifanya kifaulu, inawezekana miaka iliyopita ilikuwa ni miaka ya majaribu sana, kila ulichokuwa unakipanga kinaenda upande, sio biashara unakuta hakuna faida ambayo ulikuwa unapata. Naomba nikwambia Mafanikio sio tu kufaulu jambo ambalo ulikuwa unalifanya hata unapojaribu kufanya na ukashidwa ni mafanikio pia. Failure is the prove that’s you tried something and there is no failure without a lesson, and a lesson is AN OPPORTUNITY nikimaanisha kwamba Kufeli ni uthibitisho tosha kwamba umejaribu kitu flani na hakuna kufeli bila kujifunza na kujifunza ni Fursa.Mwaka huu unaweza kuona wenzako wanapiga hatua na wewe unazidi kushindwa. Naomba nikwambie kitu haujafeli ila unajiandaa kupokea vikubwa zaidi ya wengine mwaka huu. Mungu akitaka kukupa mambo makubwa lazima akufundishe kiukubwa zaidi. Na Mungu akitaka kukufanya kuwa Na falme juu ya falme zoote ataacha wafuasi wako watangulie abaki na wewe kuweza kukupa mafunzo ya jinsi ya kuwaongoza waliokutangulia. Muda mwingine maisha yanatupa anguko ili Tuweze kuinuka na kasi ingine.
Naomba nikupe mfano mmoja mzuri sana wa Raisi mteule wa Marekani Donald Trump mwaka 1990 alikuwa na deni binafsi la $1 Billion na kutoka katika sekta zingine alikuwa anadaiwa kama $9 Billions, jumla ni $10 Billions, hizi ni Trilioni za hela hapa, lakini alipoulizwa na Mwandishi kwamba Hauogopi?? Alijibu kishujaa Sana akasema Kuogopa ni kupoteza muda.Uwoga unaingia katika njia yangu kunisaidia kutatua matatizo.
Mwaka huu na sisi tusiogope kwa yaliyotokea miaka iliyopita lakini tutumie mafunzo ya mambo ambayo yametokea miaka mingine kutengeneza mwaka huu kuwa wa tofauti zaidi.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386586
Email ;lazarossmweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment