Monday, June 12, 2017

HILI NDILO GIZA UNALOONGOZANA NALO

Image result for LIGHTNESS IN MIND QUOTES
"Giza haliwezi kufukuza giza bali ni mwanga ndio ufukuzao giza"

Huwa tunaogopa giza kwasababu hatuoni mbele lakini kwenye giza kukiwa na mwanga hata kidogo tunapata imani na ujasiri wa kusonga mbele. Ni kwasababu gani unakuwa na uwoga na giza? kumbuka sio kwasababu unaona giza lakini ndomaana unaogopa lakini ni kwasababu ya mambo ambayo unadhani yako ndani ya giza, mfano watu hawapendi umasikini kwasababu ni umasikini lakini hawapendi umasikini kwa mambo ambayo yako ndani ya umasikini na watu wanapenda utajiri kutokana na mambo ambayo yako ndani ya utajiri.Unatengeneza giza katika maisha yako kwa kufanya mambo ambayo yako njee na wewe ulivyo na jinsi unavyotakiwa kufanya, unapenda kuwa mpishi lakini kwa kukosa maarifa unafanya mambo ya kuwa mshonaji kitakachotokea ni kwamba unaona giza kwenye ushonaji kwasababu unaona kabisa husongi mbele licha hivyo na kwenye mapishi ambako sasa unapapenda unakata tamaa kwasababu sasa hujui utaanzaje. Kukosa maarifa kukupa mwelekeo sahihi na mzuri ni giza lenyewe.Tuchangamke usiseme litaondoka tuu, hapana, ukiwa na hii kanuni ya STC itakusaidia kuondoa giza katika maisha yako na kuwa na mwelekeo sahihi ;

1. SOMA

2.TAFAKARI

3.CHUKUA HATUA

Hapa iwe kama mzunguko katika maisha yako kwamba Unasoma, unatafakari unachukua hatua baafa ya kuchukua hatua rudi endelea kusoma tena, Tafakari na chukua hatua tena.


Wengi huwa tunageuza mambo na kuwa CTS na ndo maana kunakuwa na giza haswa la kufanya mambo ambayo hatuyapendi kabisaa yani;

1. CHUKUA HATUA

2.TAFAKARI

3.SOMA

"Where your True Heart belongs is where your victory found" - Lazaro Samwel

Leo hii nakuelezea giza kwa mfano wa mtu kutokuwa na maarifa, mfano wa mtu ambaye anapenda kujiona katika nafasi zingine za maisha lakini hapendi kufanya vitu  vya kumpeleka huko anapopapenda. Naongea na wewe ambaye unadhani mafanikio yanakuja ukiwa na furaha kila siku kila muda, naongea na wewe ambaye unadhani kwamba mahusiano yako yanajengwa kwa kutokufanya makosa. Hiyo ni ishara ya kuwa na giza.

"if you want a palace be a palace" - Lazaro Samwel

Mwanga katika  maisha yako ni wewe kuwa na maarifa na haswa maarifa ya kusoma vitabu sahihi katika maisha yako sio kusoma vitabu ilimradi, kunawakati nilikuwa namsiliza Apostle Shemeji Meleyeki anasema kunarafiki yake mmoja alikuwa anapenda sana kuwa public speaker lakini cha ajabu vitabu ambavyo alivyokuwa anasoma ni tofauti na jinsi alivyokuwa akitaka kuwa unakuta ni vitabu vya kujenga ushirika, jinsi ya kuhubiri na vingine vingi, hapa unategemea kweli kama ingekuwa wewe utakuwa public speaker wakatia umeacha kusoma watu kama wakina Brian Tracy, Tony Robisons, Zig Ziglar, Kumsikiliza Mc Luvanda au Chris Mauki. Ushawahi kujiuliza kwanini Mfalme Solomoni, Paulo,Luka, Yohana na wengine wengi ambao unawajua katika Biblia waliamini katika maandishi na hawakubaki na jumbe akilini mwao ambazo leo hii tunazisoma katika Biblia licha ya kuongozwa na Roho Mtakatifu kuandika? kunanguvu katika kusoma ndomaana waliamua kuweka jumbe katika maandishi au Ukiangalia kitabu kitatifu cha Quaran unadhani kwanini jumbe ziko katika maandishi? unadhani ni kutunza tuu zisipotee au kutunza kumbukumbu?? Hapana bado tunarudi kusema kwamba kunanguvu kubwa sana kwenye kusoma. Kunaswali mmoja ambalo ningependa kukuuliza kwamba kama husomi Quran au Biblia au hata magazeti ya kuelimisha wewe utakuwa unaongea nini? jitafakari.Usishangae ukawa ni mtu wa kukimbiwa na watu.

Kwa dunia ya sasahivi inabidi nyumbani usikose kitabu cha kukubadili haswa mawazo yako, mana ndipo giza nene hupenda kupumzikia huko na usipoangalia kweli hata ongea yako inaweza kuwa ni giza kwa wengine. Watu walikuwa wanashangaa kwanini Hayati Mwl Julius .K.Nyerere anaongea kama mtabiri mpaka wengine wakawa wanasema kwamba ni mizimu ya kwao ambayo ilikuwa inafanya kazi lakini siri kubwa kutoka kwa Hayati Mwl Julius K.Nyerere ilikuwa ni kusoma vitabu sana, amekufa nyumbani kwake akiwa ameacha zaidi ya vitabu 8000, licha ya hivyo angalia John Q Benham kutoka marekani yeye nyumbani kwake anavitabu milioni 1.5, mimi na wewe inabidi tujiulize tunavingapi kwetu? je  hata wageni 20 kwako ambao wanapenda kusoma vitabu watapata vitavu vya kusoma na kuwatosha? unadhani ni kwanini vitabu tena kwa idadi kubwa sana hivi kutoka kwa Mr John Q Benham tena vyake mwenyewe? kwanini tusisome kimoja basi au kwanini tusiwe na kitabu kimoja au viwili majumbani kwetu? inamaana kukosa maarifa ni moja katika magonjwa mabaya katika maisha yetu na dawa pekee ni kusoma vitabu na kufanya tafakari sio kusoma tuu.

Mimi nimeona nikusalimu kwa Namna hii angalia na wengine usiwaache bila kuwarushia ujumbe huu hakikisha kwamba miezi hii ambayo imebaki unaanza kutengeneza Libray kwako kwaajili yako na watoto wako.


Lazaro Samwel 
0753616584 / 0653386586

Email ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment