
"Mtu atakuheshimu akiona wewe unajiheshimu na kuheshimu vile ulivyokuwa navyo" - Lazaro Samwel
Ukiona unadharauliwa jua kuna kitu ambacho unacho umekidharau au hujakifanyia kazi ipasavyo katika maisha yako. Heshima yako inaanza kwa kuheshimu ulichokuwa nacho na kukifanyia kazi sio, leo hii ukiulizwa kwanini ukikutana na Ronaldo ukikutana nae utaongea nae kwa heshima? sio kwasababu anaitwa Ronaldo ila ni kwasababu ya kitu ambacho anakifanya na kukiwekea nguvu na akili zake zote kwa heshima kubwa tuu.Ukikutana na Aliko Dangote leo hii hautaongea nae kwasababu anaitwa Dangote ila ni kwasababu ya anachokifanya kwa nguvu na akili zake zote bila kusahau kuheshimu anachokifanya.Hii ni mifano michache sana ambayo nakupa kwa lengo la kuweza kukufungua kwanza kwenye hili somo. Leo Hii unatamani kuwa kama mtu flani na unajiona kama huwezi kufika huko nikwambie kitu kimoja kwamba umekalia kitu ambacho unaweza kuwa zaidi ya yule ambaye unatamani kuwa kama yeye, tatizo lako ni kwamba unajua unachokipenda na unapenda kukianza lakini hicho kitu unachokipenda unakidogoza kwa kuangalia hostoria yako ya nyuma, kuangalia maneno ya watu, unaangalia maneno ya familia yako, unaangalia kisomo chako.Heey, amka sasa fanyia kazi hicho kitu ambacho umekinyamazia na unaogopa kukifanya. Leo hii wanakuona wa kawaida kwasababu hautaki kunyanyuka kuchukua dhahabu yako. Leo hii unakuta hauheshimiwi sana ila ni kwasababu wewe mwenyewe kunakitu hujakiheshimu ndani yako na kukifanyia kazi.
Heshima yako utaipata kwa kuheshimu mambo ambayo unaweza kuyafanya na sio kuweka nguvu na akili kwenye mambo ya watu wengine na ukasahau kwamba na wewe unamambo ya kufanya tena zaidi ya yale ambayo unapotezea muda.Ndomaana nakwambia kwamba ukiona unadharauliwa jua kunakitu ambacho umekidharau ndani yako na unakiona hakina dhamani katika maisha yako.Huu ndio wakati sahihi wa kuanza kukifanyia kazi hicho ambacho unaona hakina thamani katika maisha yako anza kwa udogoudogo unaouona na jambo lako litakuinua tuu. Ukijiona kabisaa unapenda kupika vyakula na unaogopa kuchekwa aisee amka nenda kafanya inawezekana huko ndipo mlango wako wa kutoka kimaisha unaanza, inawezekana huko ndiko heshima yako itakapoanza kuonekana zaidi.Unaweza kujiona kabisaa kwamba ukifanya kazi ya kulima utafanikiwa lakini unaogopa kwasababu ya elimu yako, amka nenda kafanyw hapo ndipo inawezekana kubadilisha historia ya maisha yako na familia yako, inawezekana unaona kabisaa kwamba nikiuza dagaa, barafu, ubuyu na vingine vingi utatoka kimaisha nenda kaanza acha dunia iendelee kushangaaa mana ni kawaida kwa walimwengu kupiga kelele kwa jambo ambalo hawaoni mwelekeo ila wewe tuu ndiye unayeona.
Kumbuka haulipii TRA kubadilisha maisha yako, chukua hatua sasa, wakati ndo huu wa kuheshimiwa na kuwa unavyotaka - Lazaro Samwel
Vimebaki Vitabu vichache kwa ofa Karibu kuwa Mmoja wapi kupata kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment