Friday, June 16, 2017

MAONO NA MALENGO

Image result for vision and goals quotes
Kunamaono ambayo yanakusaidia kuweka malengo na kunamaono ambayo unakuwa nayo baada ya kuweka malengo yako, leo naenda kukupa kitu kingine cha tofauti kidogo. Twende pamoja.

Kila kitu katika maisha yako kinachotokea ni  baada ya kutimiza picha uliyoijenga katika akili yako,leo unavojiona unahangaika sio kwasababu ya kukwepesha aibu katika jamii yako hapana ila ni picha ambayo iko katika akili yako ndiyo msukumo mkubwa wa shughuli zako zote kutumia .Ukiona malengo yako hayafiki popote ni bado hujayangea picha na malengo yoyote ambayo ukiyasoma hayakupi picha ya wewe kuwa mpya hayo bdo sio malengo,unatakiwa kuyafuta na kuangalia kutengeneza mengine. Malengo yenye maono ni sawa na kioo ambacho kinakuonesha mbele kunanini,unadhani ni kwasababu gani watu kama Albert Einstein hakuweza kumaliza high school na alionwa kama hana akili lakini aliweza kusonga mbele na leo hii anatambulika kuwa moja ya watu ambao walikuwa na akili haijawahi tokea? kwanza kabisa nikufundishe kitu kimoja kabla ya kukueleza nilichotaka kukwambia,nimegundua kwamba hakuna kosa kubwa ambalo binadamu anaweza kulifanya kama kumwambia binadamu mwenzake kwamba NAKUJUA hata mzazi wako hakujui kwa asilimia zote na kama angekuwa anakujua ingekuwa unazaliwa na unaambiwa mwanangu wewe nakuona ni daktari au wewe nakuona mhamasishaji, lakini hiyo haipo mana Mungu tu ndiye anajua alichokiumba na sio kilichoumbwa na Mungu kinajua kilichoumbwa na Mungu.Nakwambia hivi kwasababu mwalimu wa  Albert Eistein alikuwa anamjua Albert Einstein kwa nje tuu na hakuweza kuona maono ambayo Albert Einstein alikuwa anayaona katika malengo aliyokuwa nayo,usiende mbali Kuna watu kama wakina Michael Jordan unajua kwamba hata yeye alifukuzwa kwenye shule ya mafunzo ya mpira ya kikapu kwa kuwa walimuona hawezi kucheza mchezo huo? unahabari pia kwamba  Thomas Edison kunamarafiki walimuona kwamba hawezi kufanikisha kuwasha balbu? hawa walikuwa ni watu wa NAKUJUA WEWE. 

Tabia moja ambayo nimekuwa nikishuhudia katika malengo ya mtu ni kwamba kunakuwa na maono ambayo ukisema utamke kwa watu kwanza unaweza kuonekana kama kichaaa mana hakuna anayekujua zaidi ya kukuona na kuongea nawe vitu vya kawaida. Usishangae unapoanza kuongea maono yako kwa watu wakawa wanasema aisee jamaa huyu au dada huyu kaanza kuchanganyikiwa ni kawaida hiyo.Tena ukute kwamba katika familia yako au ukoo wako hakuna mtu ambaye ameshawahi kuwaza na kufanya kitu ambacho unataka kukifanya ndo unaweza shangaa utakavyosemwa na utakavyopomdwa na maneno ambayo kama kweli ingekuwa tindikali ingeshakuunguza zaidi hata kuliko maneno ya watu wa pembeni. 

SONGA MBELE HAKUNA ANAYEKUJUA ZAIDI YA MUNGU WAKO NA HESHIMU MAONO YAKO AMBAYO UNAYAONA KATIKA MALENGO YAKO. ILA MWENZANGU NAPENDA KUKUSHAURI USIMDHARAU MTU KWASABABU HAUMJUI PIA. 

"Kuwa na wakati mzuri. Usichoke kuwa mabadiliko katika maisha ya watu wengine. Mana mabadiliko ya wengine ndiyo mabadiliko yako" - Lazaro Samwel 

Lazaro Samwel
0753616584 / 0683539684

Email ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment