1.
Wakati umeshafika, Vijana tukaamka
Tuache kulalamika, Fursa tukazishika
Nguvu tunazo hakika, Tusiwe wa kubweteka
Akili zikatumika, Uchumi bora kuweka.
2.
Vikundi tukaviweka, Kwa umoja tutafika
Tukaenda nakufika, Majembe tukayashika
Kazi sera imefika, Shambani pakachimbika
Ajira zisipotoka, Akili huchangamka.
3.
Mvi hazijatufika, Muda nguvu tukaweka
Kazi tukashughulika, Fedha halali kushika,
Uvivu wa kuamka, Na mwilini kututoka
Vitanda tukavyondoka, Kulitupa nalo shuka.
4. Tusome
sana hakika, Kesho picha tukaweka
Ipo siku itafika, Chuoni tutaondoka
Mambo yakakamilika, Uzembe ukatuvuka.
Tusione tumefika, Vijana tukabweteka.
5.
Sisi tunahitajika, Jamii kuchakarika
Vipaji vikatumika, Na nyimbo zikaimbika
Vitabu tukaandika, Hazina kesho kuweka.
Vilevi mbali kuweka, Mwili wapata kuchoka.
6. Nguvu
nyingi kuziweka, Na kazi kumalizika
Mengine mwili wachoka, Safari kutoifika
Busara nazo kushika, Uzee tukaufika
Kwa Nguvu tunasifika, ni heri zikatumika.
7.
Kituo nimekifika, Nasaha kuzikumbuka
Mvi na zitatufika, Sisi tusipoamka
Muda utatuponyoka, Tusiweze kuushika
Tuache tu kutamka, Vitendo
visofanyika.
Raymond
Nusura Mgen.
0766461571/0676559211
0766461571/0676559211
Mgeniraymond@yahoo.com/raymondpoet@yahoo.com
Chuo Cha Kumbukumbu Hubert Kairuki
Chuo Cha Kumbukumbu Hubert Kairuki
0 comments:
Post a Comment