Sunday, May 28, 2017

NYANYUKA UANZE TENA

Tokeo la picha la rise and shine quotes
1.       Kuanguka sio mwisho, nafasi ipo nyanyuka
Sio lake hitimisho, huwezi tena inuka
Lipo lingine amsho, taa kuweza kuwaka
Naweza liwe tamsho, hatua mpya kushika.

2.       Chombo kiharibikapo, sio mwisho wa safari
Na Haiishii hapo, mtu kukata shauri
Taa yaweza wepo, kukupa namna ari
Mivumo ivumapo, Moyo utabaki shwari.

3.       Siku haibaki leo, siku nazo husogea
Usichoke kwayo leo , kuyafanya endelea
Waweza kufanya leo, kujenga nzuri tabia
Yafikapo na machweo, ishara siku kwishia.

4.       Jitie na huo moyo, alivyo mpiga mbio
Kufanya mambo yaliyo, yakusogeze upeo
Juhudi iseme ndiyo, kama ilivyo chepeo
Mshairi yangu hayo, chanya uwe mwelekeo.

Na Raymond Mgeni
.0766461571/0676559211
Chuo cha Kumbukumbu Hubert Kairuki..Mikocheni

Mgeniraymond@yahoo.com/raymondpoet@yahoo.com 

0 comments:

Post a Comment