Monday, May 29, 2017

KUNA MAMBO TUMESAHAU?


 Tokeo la picha la quotes about the problem of most african resource utilization

"Hakuna mtu masikini wa pesa ila sisi wenyewe ndio ambao tunatengeneza watu masikini. Kuna watu ambao leo hii wamekosa pesa kwasababu ya muonekano wa mawazo tenganishi baina ya watu wenye pesa na watu ambao wenye nazo lakini sio zaidi ya watu ambao wanasemekana ni matajiri duniani. Nakwambia hakuna masikini kwasababu kama kwenye 100-50 = ni 50 au 10,000/= -5/= ni 9995 basi hata yule ambaye leo hii unachukua kidogo chake katika biashara na kukufanya wewe kuwa tajiri na yeye ni tajiri lakini umemzidi kiwango ambacho dunia nzima inachukuliaWewe kuwa tajiri na yeye kuitwa masikini" - Lazaro Samwel

Na ni kweli kunamambo ambayo tumesahau ndo maana hata ushindani ambao tunakuwa nao sio ushindani wa kwetu wenyewe lakini ni ushindani wa kuangalia flani kafanya nini au nchi flani imefanya kitu gani na sisi tuweze kufanya kuipita.Kwa maoni yangu ni kwamba tunakosa kitu kimoja haswa ni kuongozwa na falsafa ambazo hatujazifanyia tathmini katika maisha yetu ila kwasababu imekuwa tukizifuata  kwasababu zinatuletea matokeo sawa na watu ambao wanasifika dunia basi tunaona ndivyo maisha yanavyotakiwa kuwa. Mfano Tanzania angalia wangapi wanahangaika kuleta taswira mpya ya wao kuwa wao na ijulikane kitu flani kimetokea Tanzania? Ni wachache sana, laiti kama ingetokea Tanzania au Africa tukatumia mawazo yetu baada ya kujua  wengine wanawaza nini naimani na wao pia wangekaa na kuwaza Tanzania au Africa kunanini ila kwa kuwa hatuna Muda huo ndo mana kila siku ni Marekani wamefanya nini? Arsenal wamecheza na timu gani, matokeo yake yalikuwaje?  BMW wametoa aina gani ya gari? Kampuni ya Apple imetoa simu gani tena?  Beyonce kafanya nini? Kevin Hurt Kafanya nini? N.k vipi unajua kuhusu kiwanda cha Nguo Arusha? Umeshawahi kununua hata nguo yao moja au unawahi Vitu vya Gucci? Je unajua kuhusu kiwanda cha kutengeneza Maziwa TANGA FRESH? Au ndo kwanza unawahi kuchukua maziwa kutoka Dubai, Marekani?  Huku ndipo mambo yanapoharibikia kwamba inaishi Afrika tena Tanzania alafu unatumia vitu ambayo sio vya Tanzania.


Tanzania haina tu vivutio vya wanyama wengi kwa watalii kuangalia lakini kunampaka vivutio vya watu wengi ambao wanapenda Tanzania ibadilike lakini hawapendi watu wanaotaka kubadili Tanzania,watu ambao wanapenda kusikia Bill Gates kuwa bilionea namba moja Duniani kati ya mabilionea 1826,lakini wakisikia kwamba Kunamtanzania flani anafanya juhudi za kuwa moja ya mabilionea cha kwanza wanamchukia na wanachukia pia kwa kusema anaringa.Hivi ndivyo vivutio vingine ambavyo vinongeza utalii na pato la Tanzania kwa watu kuja kutushangaa kwamba Tanzania na rasilimali nyingi walizokuwa nazo kwanini hakuna mabilionea? - Lazaro Samwel

Lazaro Samwel
Contacts ; 0753616584 / 0653386586
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

Facebook Page ; Lazaro Samwel
Instagram         ; Lazaro Samwel3 

0 comments:

Post a Comment