1.
Jana umeniambia, leo niingoje kesho
Nami
nikakusikia, wasema niende mwisho
Nami pasipo
kujua, nikasema huu mwisho
Kwa raha
nikatulia, ‘kisema nafanya kesho.
2.
Wengi umewaambia, waingoje hiyo kesho
Nao pasipo
kujua, wakidhani hitimisho
Wengi na
wakatulia, wakiisubiri kesho
Leo wakazitumia, sijue kupata kesho?
3.
Mvi na
zikanijia, kukusubiri we’ kesho
Nguvu
zikaniishia, ahadi nifwate kesho
Jina hadi
‘kafifia, wasema nafasi kesho
Kifo hadi
chakaribia , waagiza nije kesho.
4.
Hadi Nikaulizia, bei yako wewe kesho
Wenda
ningekununua, usitwaje tena kesho
Kwani
kutoniambia, nipajue kwako kesho?
Njia hata
sikujua, u mwongo sana we kesho.
5.
Sasa hadi ‘mejifia, ndoto eti ipo kesho
Hadi
vikajiozea, tumai huenda kesho
Busara yenye
tamaa, hukusema iwe kesho
Lini
utatuambia?. wapi uishipo kesho?
Na Raymond
Nusura Mgeni..
0766461571/0676559211
Barua pepe:
mgeniraymond@yahoo.com/rqymondpoet@yahoo.com
0 comments:
Post a Comment