Sunday, May 28, 2017

SUBIRA YAVUTA HERI

Tokeo la picha la patient  quotes
      1. Usichoke kusubiri, malenga nawakumbusha
   Usichoke kutabiri, ya kesho bora maisha
   Usiache tafakari, mambo kuyaimarisha
   Uishi na watu shwari, furaha yawe maisha.

      2.  Endelea kupambana, iwe usiku mchana
   Mazuri ukayanena, macho mazuri kuona
   Kama u bado kijana, andaa nzuri hazina
   Usishi mambo ya jana, leo kushindwa kuona.

          3.  Panda mbegu zile nzuri, iko siku utavuna
  Kwanza kuota subiri, zitamea utavuna
  Nawe kama u mshairi, vitunge vizuri vina
  Usichoke kusubiri, mbegu ulopanda jana.

     4 .Uzuri siku zaenda, masaa yanasogea
  Anza maisha kupenda, vizuri kujiishia
  Anasa kutozipenda, hukatisha yako nia
  Hekima itakulinda, itakuongoza njia.

5.Siku ipo vitakuja, leo unavyojifanyia
  Uzuri wakati huja, hata ukisubiria
  Kutimiza yako haja, kujifunza kutulia
  Jenga nzuri zile hoja, ijao kufurahia.

6. Malenga namalizia, subira yavuta heri
  Usache  kung’ang’ania, moyo ule wa saburi
  Utaipata na njia, usipoileta shari
  Vina vimeniishia, mwisho nakata shauri.

Na Raymond Mgeni
0766461571/0676559211
Chuo Cha Kumbukumbu Hubert Kairuki
Mgeniraymond@yahoo.com/ raymondpoet@yahoo.com


0 comments:

Post a Comment