Sunday, May 28, 2017

FUNZO KUHUSU FEDHA


Tokeo la picha la money quotes
Habari mpenzi mfuatiliai wa Application ya LAZAROSAMWEL.Leo hii Mwl Victor Deogratias kutoka chuo cha SAUT Mwanza anaenda kukushirikisha somo zuri sana kuhusu Fedha.Twende Pamoja.

Watu wengi wamekua wakilalamika juu ya fedha.Watu wanalalamika hawana mtaji.Watu wanalalamika fedha hakuna.Je ni kweli huna mtaji?. Katika kujifunza somo hili fupi sana ila ninalotamani liwe na matokeo makubwa sana kwako nataka ujiulize maswali haya;

  • Huwa napokea shilingi ngapi kwa mwezi?( kama ni muajiriwa)
  • Huwa naingiza faida kiasi gani kama faida?( kama ni mfanya biashara).
  • Huwa napewa kiasi gani kwa wiki,mwezi?( kama ni mwanafunzi)
  • Huwa ni fedha kiasi gani inapita mkononi mwangu kwa kupewa?( hizi ni zile bonus  umepewa na shangazi, rafiki n.k).

Baada ya maswali hayo nataka ujue jambo hili kwanza.Hakuna ela ndogo wala ela kubwa.Nasema hivi kwa sababu sh 100,000 imetengenezzwa na sh 10,000 kumi, sh 1000 mia moja na sh 100 eflu moja.Lakini pia hakuna ela itakayokuja kukutosha, ni mpaka ufikie kiwango umeshindwa kuhesabu ela zako kwenye akaunti yako.Kama una uwezo kutaja kiwango cha ela ulizo nazo kirahisi ujue hujafika.Sasa lengo langu ni nini?

Lengo ni hili.

Kitabu cha hekima ninachokitumia sana kinasema

" Mpumbavu hutumia vyote bali mwenye akili huweka akiba"

Hapa watu wengi wamefeli, mtu anapata sh 1000 anafikiri ni ndogo ananunua soda na keki, anangojea siku apate sh 1,000,000 angalau aseme hii nyinginyingi kidogo.Ngoja nikwambie; kama umeshindwa kutunza sh 300 kwenye 1000 hutaweza kutunza 300,000 kwenye 1,000,000.Kwa nini? Ni kwa sababu binadamu mahitaji yake hayana mwisho ila fedha ina kikomo.

"Wants are unlimited and money is scarce"

Usipojifunza nidhamu ya fedha, sahau utajiri. Hii ni kwa muajiriwa, mfanyabiashara na ambaye haujaanza chochote.Leo unalia huna mtaji ila nikikuuliza mwaka jana umetumia shilingi ngapi utanipigia hesabu na yamkini ikawa mamilioni mengi sana na kati ya hayo utakuta safari zisizo na tija, lunch za gharama ambazo hazikua na ulazima, nguo ili uwe smart ila hukua na kiasi na mengine mengi. Simaanishi kwenda out ni kubaya au kuvaa vizuri, hapana. But rembember this" It is not expensive to look smart" ni maamuzi yako. Na si kila kitu lazima ukifanye, jifunze kuweka vipaumbele.Kati ya ela iliyopita kwenye mkoba, pochi yako, ni sh ngapi umetunza ili uwekeze au ufanyie biashara?Naongea jambo ninalolifanyia kazi.Tangu nikiwa mwanafunzi na hata sasa nafanya kazi, kila ela niliyokuwa napata 20% ilikua ni akiba ya kuwekeza. Na fursa za ela zote zilikua zinanikuta na akiba ndani.Nilifika kipindi cha kubaki na sh 100 ya matumizi ila nina 300,000 ya akiba ya uwekezaji na iko ndani.Sisemi kujivuna, ila nataka nikuoneshe kuwa inawezekana.

Nafanyaje ili niwe na nidhamu ya fedha? (Nitakuekekeza mbinu ninazotumia).

Kuwa na mkakati wa kukata asilimia fulani kwenye kila unachokipata. Namaanisha kila unachokipata kasoro mkopo, ada na ela ya watu. Ila hata ukipewa ela ya pongezi 10000 kata asilimia ya akiba, ukikutana na mimi nikakupa 2000 kata ela ya akiba. Usidharau ela yoyote. Nimelithibitisha hili.Wekavipaumbele. Sio kila sherehe (party)  lazina uende, sio kila sehemu lazima uvae nguo mpya, sio kipodozi lazima ukitumie sasa, sio kila msuko lazima usuke nyakati hizi, sio kila jeans zinazoingia lazima uvae, sio lazima  kula hotel za bei wakati iko migahawa inauza chakula kizuri na bei nafuu.Unapotaka kununua kitu, nunua kimkakati, sio unanunua kitu ambacho utatakiwa kununua tena mwezi ujao. Mfano unaenda kununua kitanda unajua kuna siku utakua na wageni, utaoa. Unanunua 4*5 kisa ndo saizi yako, kuna siku itakugharimu kununua kingine, utakua umepoteza ela fulani.Nunua rasilimali na sio madeni. Kuna watu wananunua madeni. Mfano anapata ela nyingi ila anaishia kununua ving'amuzi, anajiunga bando za kutumiwa story na vodacom, kutumiwa nyimbo na anakatwa ela, king'amuzi sio kibaya maana unapata taarifa, ila yatambue majira uliyopo na unachokihitaji. Nilinunua kiwanja nikiwa niko chuoni na sina kazi, ningeweza kununua flat screen.Weka vipaumbele, panga mambo yako ili ela inapokua unaigawa kwanza kwenye mambo ya msingi.

Ukiona huwezi kukaa na ela, iweke mahali ambapo itazaa, na hili ndo lengo. Kama hujapata wazo la biashara la kufanyia kazi, tafuta mahali pa kuiweka ela yako itakapozaa, ukikaa nayo itakushawishi kuitumia.

Nilikua ela yangu inafika zaidi ya laki 200,000 nikiwa chuoni, nilipeleka kwenye vikundi vya akina mama, nakopesha narudishiwa riba 20%.Sasa hivi nafanya kazi, nikipokea mshahara, nakata 20% ya kuwekeza hata kama nina shida kiasi gani,na ninampa mtu anaenda kufanyia biashara anarudisha 10% nimefanya hivyo.Kwa hiyo ndugu yangu, usilalamikie serikali kuwa huna mtaji, ela ambayo ushakula ungekuwa unaweka akiba na kuwekeza ungeshafika mbali. Umeshindwa vipaumbele.


Mr.Victor Deogratias 
Contacts ; 0758719242
Email     ; victordeogratias21@gmail.com

0 comments:

Post a Comment