Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel,nikiwa naimani u mzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku.Napenda kukupongeza kwa kuendelea kuwa mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa makala hizi za kila siku ambazo zimelenga kumbadilisha mtu kuanzia ndani na kujiona kwamba anaweza kufanya kitu ambacho anapaswa kukifanya katika maisha yake bila kusahau kutimia vitu ambavyo vinamzunguka kwa manufaa yake na jamii yake pia.TWENDE PAMOJA.
Ningependa kwanza kuweza kukufungua kuhusu rasilimali, Nini
maana ya Rasilimali?Rasilimali inaweza kuwa watu, pesa, mashine yako, ardhi na
vitu ambavyo unaweza kuvitumia kukuletea matokeo flani mazuri katika maisha
yako.Inawezekana ukawa unashangaa kwamba kwamba watu wanakuaje rasilimaliila
kumbuka kuna kitu kinaitwa Rasilimali watu, inaweza kuwa watu ambao umewaajiri
kuhakikisha kazi yako inatendeka au watu watu unewaweka kuendesha rasilimali
ingine kama mashine katika kiwanda chako au kampuni yako. Leo nitapenda kwa
kifupi ili nihakikishe kwamba huu ujumbe unakufungua vizuri.
Zifuatazo ni sababu za
kushidwa kutumia rasilimali zako vizuri ili uweze kufanikiwa.
1. Kuwa Na Visingizio
Hakuna kibaya kama kuwa na visingizio na ukitaka hata usione
kitu flani kinadhamani weka visingizio mbele. Visingizio huwa vinabadilisha mtu
macho yake kuwa kama ndo akili na akili kufungwa kuona mbele pakoje. Angalia
watu wengi ambao wanavisingizo na wanahela nzuri tuu au wanamshahara mzuri tuu
siku zote kuishia kuwa masikini au kuishia na maisha mabovu. Visingizio lengo
lake ni kwamba kuacha kushughulikia swala lako sasahivi ukidhani kesho ndipo
utaliweza kulifanya lakini inakuwa uwongo kwasababu hata kisingizio chenyewe hakijui
kesho yako. Hakikisha kama unamalengo mazuri na rasilimali nzuri usiiwekee
kwamba kesho utaitumia anza kuifanyia kazi. Ukiipa kesho na inawezekana kesho
ilikuwa iwe na matokeo mazuri na utakuwa umepoteza thamani yake.(Hii point
nitaiunganisha na point ya mwisho kulandana vizuri)
2. Kutokuwa Na
mtizamo chanya kwa rasilimali ambazo zinakuzunguka.
Ubongo wako ukijaza mambo mabovu usishangae kutofanya mambo
mazuri, na ukitaka kujibadilisha anza kutoa huo uchafu wa mawazo hasi na kuanza kuweka mawazo chanya ambayo
yatatokana na rasilimali ambazo unazo.
Hapa mara nyingi watu
huchukua historia ya kitu flani ambacho alisikia kwa watu wengine na kuona kama
ndo yeye. Ndugu unajipoteza, kumbuka huyo ambayo umewazia kilichotoea sio hata
wewe na yeye sio wewe, wewe unafamilia yako na yeye anafamilia yake kwa kifupi
kila mmoja anamaisha yake na hayawezi kufanana.Sasa unaporuhusu mawazo hasi
kupitia maneno ya watu nakwambia haya rasilimali ambazo unazo utazitumia vibaya
zaidi hata kama zilikuwa nzuri na zingeluletea mafanikio makubwa kwako.Acha
tabia ya kuwa na mawazo hasi kupitia historia ya watu wengine jiangalie
kivingine kutoka na maono yako yalivyo pamoja na malengo yako kupitia
rasilimali ambazo unazo.
3. Kutokuthamini
Muda.
Unaweza kuwa na rasilimali za aina zote, ukawa na malengo
mazuri sana lakini ukiwa hujui thamani ya muda katika kuhakikisha unatumia
rasilimali zako vizuri hauwezi kufika sehemu yoyote katika maisha. Mafanikio
yako hayatapimwa kwa kiwango cha rasilimali ambazo unazo ila ni kwa jinsi
ulivozitumia rasilimali zako kwa muda sahihi sehemu sahihi pia.Ukiona pesa yako
haifanyi chochote angali unaiendeshaje sambamba na muda? Muda ni pesa( Time is
Money) Hii sehemu ni pana sana sana ila cha msingi ni kwamba ukitaka kutumia
rasilimali zako vizuri hakikiha unaenda na muda na usiwe mtu wa kuairisha mambo
kwa kwa kudhani kwamba mambo yanakusubiri. Ndo maana kunatofauti kati ya
usafiri wa gari na usafiri wa ndege watu matajiri huwa wanatumia ndege kuokoa
muda sio kwamba wanapoteza hela, hapana, wanaangalia muda kwamba mfano kutoka
Mwanza mpaka dar inaweza ikawa mpaka kesho lakini nikitumia fasthet ni 45
minutes, kwahiyo unamaana kama ni kufanya biashara zako unafanya na kurudi na hata ikiwezekana unaweza kusafiri sehemu
ingine kufanya biashara ingine pia ikiwe yule mwingine bado yuko safarini.
4. Kutokuwa Na
Maarifa.
Hakuna sehemu ambayo unaweza kufanya bila kuwa na
maarifa.Unapoamua kuanza na kuacha visingizio. Weka maarifa kwanza katika
kutumia rasilimali zako. Hakikisha kwamba jinsi inavoendelea kuitumia
rasilimali yako pia unaendelea kutafuta maarifa zaidi mbele yake. Lakini kama
utaamua kuanza lakini huna maarifa
utasogea mbele lakini sio kama jinsi ungekuwa na maarifa zaidi. Soma vitabu
sana ukajua jinsi ya kuongoza rasilimali ulizokuwa nazo na kuzielewa vizuri
zaidi kadri aiku zinavozidi kwenda.
Kuwa makini na matumizi ya rasilimali ambazo unazo na hakikisha kwamba hauzitumii kukuletea manufaa ya muda mfupi lakini hakikisha kwamba unatumia rasilimali zozote ambazo unazo kwa manufaa ya muda mrefu na jamii yako ambayo inakuzunguka.
SOMA; KWANINI UNATAKIWA KUSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA
ASANTE SANA KWA MUDA WAKO NA MUNGU AKUBARIKI,ulikuwa nami;
LAZARO SAMWEL Mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA .
CONTACTS ; 0753616584 / 0653386586
EMAIL ; lazarosamweli41@gmail.com
Mawazo mazuri bro
ReplyDeleteKaribu sana Stephen!
Delete