"Kama hamasa yako ni hela ili uweze kufanikiwa unatakiwa kujipanga upya katika kitu chocchote unachokifanya".
Hamasa ya kweli iko katika malengo ambayo umejiwekea haswa malengo ambayo yanakuwa na mwelekeo sahihi katika kuhakikisha unafika sehemu sahihi katika maisha yako.Ukiangalia kwa asilimia kubwa watu wengi ambao wanatumia hela kama hamasa yao ya kusonga mbele muda mwingi huwa hawafiki katika sehemu wanayoitaka katika maisha yao kwasababu leo wakipata kesho wakikosa ile hamasa inapungua na kama wakipata changamoto flani huwa wanasubiri mpaka wapate pesa ili waweze kusonga mbele katika jambo wanalotaka kulifanya.Malengo yako yakiwa ni hamasa na ukayafanyia kazi kweli kwa moyo wako wote nauhakika lazima hela ambazo unazitaka zitakuja lakini hamasa ya hela ambayo haina malengo sio kitu na mtu utakuwa na tabia ya kuhairisha mambo yako kila muda mpaka upate hela ikiwa kuna mambo mengine unaweza kuendelea kuyafanya hata kabla hujapata hizo hela kama hamasa kwako.
Nikupe kitu kimoja hamasa ya malengo yako itakusaidia kuvuta watu sahihi katika maisha yako kukupatia hela ambayo unaitaka ili uweze kusonga mbale zaidi na malengo yako na kuweza kuyatimiza kama ulivyokuwa umepangilia.
Jitahidi kujiandikisha katika program hii ya AKILI YA USHINDI tuweze kuwa pamoja kwa mwaka 1;https://akiliyaushindi.com/jiandikishe
Coach Lazaro Samwel
0753616584
Email; lazarosamweli41@gmail.com
nakuelewa san kaka
ReplyDelete