Mungu akikuinua usisasahau kuinua na wale ambao wako sehemu flani ya chini ambayo ulikuwepo hata kabla ya kuinuliwa.Kwasababu ya utandawazi na binadamu kufungwa kifikra tukishainuka tulipokuwa kwenda sehemu zingine huwa tunasahau kutumia matunda ya kuinuliwa kuinua wengine wenye juhudi na nidhamu za kutaka kuinuka kama sisi.Muda mwingine huwa nawaza na kusema kutokukomaa kifikra ni pale unapokuwa na uwoga wa kukaa na watu walioko chini ukidhani utakuwa kama wao,naamini ukikomaa kifikra watu 10 ambao wanamawazo hasi kuwabadilisha kwako haitashindikana na hata wao kukuambukiza uhasi wao itakuwa ngumu kutokana na tabia utakayokuwa unawaonesha.Huwa napenda kutumia mfano wa Yesu na Mtume wao waliwezaje kusambaza neno la Mungu na kusababisha kuwe na dini ya Kikristo na ki-islamu ikiwa katika nyakati zao walipingwa sana? jibu ni kwasababu ya kukomaa kifikra na kujua wajibu wao tena mfano Yesu hakuchukua watu maarufu ili neno lake liweze kueleweka wala hakutaka watu maarufu kumwelewa ili kila mmoja amwelewe lakini aliinua watu wa chini kabisa,angalia mitume wake 12 aliowachagua walikuwa na umaarufu sana?
Ukikomaa kifikra hutakuwa na uwoga wa mawazo yako kupotea kusema utumie watu maarufu ili uhai wa mawazo yako uwepo.Haukatazwi kutumia lakini uhai wa mawazo yako pandikiza kwa watu walioko chini yako na ukiweza kuwainua mawazo yako yataishi.Kuna muda jitoa nje ya boksi kidogo na jiulize kwamba kuna umuhimu gani mtu mwenye fikra chanya kukaa na mtu mwingine mwenye mawazo chanya ikiwa jamii yake inawatu wengine wenye mawazo hasi na wanahitaji mabadiliko? Na unawezaje kuzalisha watu wenye mawazo chanya ikiwa wote wenye mawazo chanya mwajivuna kuwa mbali na wenye mawazo hasi? Ni lazima muda mwingine mchanganyike na wale wa hasi kusudi muongeze zao la watu wenye mawazo chanya.Ndio maana hata ujio wa Yesu haukuwa mahususi kwa watenda mema ingekuwa ni hivyo asingekuwa anajichanganya na watenda dhambi.BADILI FIKRA KWA UPANDE MWINGINE PIA.
Kama bado hujajiandikisha kwenye blog ya Akili Ya Ushindi bonyeza;https://akiliyaushindi.com/jiandikishe
SIJAANDIKA UNIKUBALI MIMI NIMENDIKA UJUMBE HUU UONE THAMANI HATA YA WALIO CHINI YAKO NA WENYE NIDHAMU YA KUTAKA KUFIKA SEHEMU FLANI ULIPO.
Coach Lazaro Samwel
0753616584/0653386586
Email; akiliyaushindi17@gmail.com
0 comments:
Post a Comment