Kwa nyakati hizi ni nyakati ambazo zimejaa kelele za kila namna kwa kuwa kila mmoja amekuwa na uhuru wa kusema anachota kukisema,lakini wewe mwenye masikio ndiye mwenye chaguzi ya kusikiliza kelele zote au kumsikiliza mtu mmoja? Kelele hizi nazo kwambia sio kelele za kuongea tu, hata kwenye mitandao kuna kelele nyingi sana haswa kuwa na habari za kila namna na kuwa na taarifa za kila namna pia. Kuna wengine wanashindwa kusonga mbele katika maisha yao kwasababu wameshabeba tabia za kelele hizi katika maisha yao. Inawezekana ukawa unajiuliza nakwambia nini lakini ngoja nikupe siri moja ambayo inawezekana ulikuwa hutambui, mtu huwezi kuelewa nini kinasemwa kwenye kelele hivyo hali hii inakupotezea mwelekeo wa nini cha kujibu yani unachindwa kusikiliza kitu kimoja na kukijibu ndivyo hata maisha yetu kwamba yakisha kuwa na kelele nyingi zisizokuwa na maana hata mwelekeo wa maisha yetu hatuwezi kuujua kwasababu utafuata huku utaona tena sehemu ingine utahairisha na kufuata ingine. Kuna wengine hata wamekosa biashara ya kufanya kwasababu wako katika kelele.Lakini tatizo inaweza kuwa nini mtu kufuata hizi kelele na nini anatakiwa kufanya kuweza kujikomboa katika maisha yake?
1. Kutokutambua unataka nini katika maisha yako ni sababu kubwa sana ambayo itakufanya uwe mtu wa chochote kinachojitokeza ni chako au utaenda nacho sawa. Nikushauri kitu kimoja kwamba usithubutu kutoka katika umati wa watu kuwasikiliza kabla ya kujua unataka nini katika maisha yako kwasababu unaweza kujikuta hata ile akili yako ndogo ya kujua unataka nini katika maisha yako ukaipoteza kabisa,lakini ukishajua unataka nini katika maisha yako utajua yupi wa kumsikiliza na yupi wa kumfuata.
2. Kukubaliana na hali ngumu ya maisha aliyokuwa nayo.
Ukishakubaliana na hali mbaya uliyokuwa nayo hauna tofauti na kujiacha mwenyewe kuwa chombo cha kuwekea uchafu kwasababu unavyokubaliana na hali mbaya siku zote sio kwamba unakimbiza hilo jambo lako baya japo ni kuacha hali yako mbaya kukaribisha hali zingine ngumu na mbaya katika maisha yako. Na kwa hii hali utakuwa tayari kusikiliza kelele za kila namna katika maisha yako. Achana na hali ya kukubaliana na kila hali ngumu unayokumbana nayo kwasababu utakachokikaribisha ni kelele ambazo hautaweza kuzielewa katika maisha yako.
3.Kuilaza nafsi ya maamuzi ndani yako au kutokuwa kiongozi katika maisha yako.
Unapokuwa kiongozi unajua ni wapi natakiwa kusikiliza na wapi hutakiwi kusikiliza. Hata sehemu gani natakiwa kusoma kitu flani na kwasababu gani pia. Katika maisha yako lazima uwe kiongozi wa kujua nisikilize watu gani na kwasababu gani sio kila kitu usikilize hata vile ambavyo kabisa unajua hakuna matokeo mazuri.
Ziko nyingi sana lakini kwa leo naomba niishie hapa na inabidi ujiulize wewe katika maisha bado unasikilia kelele za namna gani ukianzia kwenye mitandao ya kijamii, mazingira unayoishi n.k jiulize jee ni sahihi kuzisikiliza? Na zimekusaidia nini mpaka sasa? Kama hakuna chukua hatua ambazo unadhani zitakusaidia kuliko kuendelea kusikiliza kelele ambazo hazikuongezei thamani yoyote katika maisha yako.
Kama bado hujajiunga na program ya AKILI YA USHINDI unaweza kubonyeza link hii https://akiliyaushindi.com/jiandikishe Kuweza kupata maelekezo ya kujiunga.Kwa wewe mwajiriwa,ambaye hujaajiriwa, mwanachuo, kijana n.k nakusihi hii program sio ya kukosa.
Ulikuwa nami;
Coach Lazaro Samwel
0753616583/0653386586
Email; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:
Post a Comment