Friday, September 8, 2017

UKICHOMOZA USISITE KUKUA


  • Mpe mtu uhuru ataonesha ubunifu,mkatishe tamaa  utamtoa nje ya kusudi lake.Haswa yule anayechimbukia katika kusudi lake.

Kuna tofauti kubwa kati ya mbegu kuwa ndani ya ardhi na kuchomoza kwenye ardhi.Mimi na wewe kufanya tunachokifanya ni kwasababu ya uvumilivu wa mambo ya nyuma kabla hata ya kuanza kufanya tunachokifanya au kabla hata ya kuonekana kwa tunachokifanya.Mbegu istahimiliyo kila hali chini ya ardhi ndiyo ichomozayo kukua na kuzaa matunda mazuri.Jifunze kitu hapa ndani ya ardhi mbegu hupata changamoto sawa na sisi tunapohitaji kukua katika mambo ambayo tunayafanya tutapata changamoto kutokana na tulipo.Changamoto zitakuwa ngumu lakini ukijipa moyo na ukasonga mbele kwa kutowasikiliza wakatisha tamaa utaanza kuchomoza kama mbegu ichomozayo kwenye ardhi.Nakukumbusha tena kwamba utakapoonekana jua kuna wengi ambao wanaoonekana kama wewe na wanaotaka kuonekana zaidi yako kwahiyo watafanya kila njia kuhakikisha uwepo wako hautambuliki kabisa japokuwa umeshaonekana.Nikupe siri moja masikio yako hayakuumbwa kusikiliza vitu ambavyo sio sahihi ila ni kusikiliza kilicho sahihi kusudi ufanye maamuzi sahihi,akili yako haijawekwa au kutengenezwa kuweka vitu ambavyo sio sahihi, kwa kifupi viungo vya binadamu vimeumbwa kwa ushirikiano kumsaidia mtu kulisaidia kusudi lake kuwa bora kama Mungu mwenyewe alivyomwumba kwa ubora.Wale wanaotumia vibaya viungo vyao kwa kuwa juu zaidi ya wengine huitwa wakatisha tamaa na ndio ambao tunaweza sema ni changamoto za mbegu iliyobora inapokuwa ndani na nje ya ardhi.Kama umeshachomoza usisite kuendelea kukua lakini tambua wapi unataka kufika sio wangapi unataka kuwapita.

Tembelea www.akiliyaushindi.com sehemu ya MENU kuweza kujisajili kwenye Program ya AKILI YA USHINDI kwa mwaka mmoja. Nakusihii ewe mwanafunzi,mwajiriwa,ambae hujaajiriwa,mfanyabiashara,mjasiriamali n.k hii program usiikose.Share na wengine pia.

Coach Lazaro Samwel
0753616584/0653386586
Email:lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment