Sunday, August 13, 2017

TENGENEZA UMOJA KATIKA MAHUSIANO YAKO

Mahusiano yasiyokuwa na majukumu ambayo yataweza kuwaweka watu pamoja ni kazi bure.Haswa yanaweza hatarisha mawasiliano mabovu kwasababu kila mmoja atakuwa anafanya mambo yake na hatakuwa na ile hari ya kumshurikisha mwenzake.Hakuna kitu kizuri kama watu wawili waliounganika pamoja wake na kitu kimoja ambacho ni kikuu kwao ukiacha na shughuli binafsi ambazo kila mmoja anafanya ili kuweza kuimarisha mahusiano haswa katika mawasiliano.

Kutokuwa na majukumu kama wapenzi au wanandoa ni rahisi hata shetani kuingia katika kuweza kupandikiza mbegu ya chuki baina yenu kwasababu hakuna kitu ambacho kinawaweka karibu.Japo lengo la Watu kuungana nikuweza kuziba mapungufu ambayo kila mmoja anayo lakini hivi vyote ni lazima kuwe na Muunganiko mzuri baina ya watu haswa katika mawasiliano na kupeana Muda pia.

Lazaro Samwel 
Life Coach 

Email;lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment