
🔰Dharau haziwezi kuwa na faida kwa mwenye dharau bali kwa anayedharauliwa. Anayedharauliwa hawezi kupata faida ya kudharauliwa akimdharau anayemdharau, mana wote watakuwa na dharau. Uzuri wa kudharauliwa ni kwamba humfanya Mungu kukuinua zaidi ya anayekudharau mana asipofanya hivyo ni Mungu ndiye atakuwa anadharauliwa sio tu yule anayedharauliwa mana Mungu wetu ni mshindi na ametuumba kwa mfano wake. Haloo, naomba ukumbuke Mungu ni mchapa kazi kwa Maarifa na hekima kwahiyo acha watu wakudharau kwa kitu ambacho unakifanya kwa maarifa na hekima, wewe PIGA KAZI,hesabu dharau kama BARAKA kwako.
🔰Sisi wote ni binadamu na tunapitia vipindi tofauti katika maisha kama shida na matatizo mbalimbali ni kawaida kutokea lakini hivi vyote kuvipa muda kuviwaza kwa jinsi vilivyo hasi ni kuvikuza na kuvitengenezea makazi ndani yetu. Vikija tukubali kuja lakini tusikubali viishi ndani yetu hata siku moja. Mambo yote ambayo yanafanya Moyo wako kuteseka ni USAFIRI WA SHETANI kuja kukuangamiza. Chukua usafiri mwingine wa Kuvitawala hivi kwa UPENDO na KUVISEMESHA kwamba ni sawa kuja lakini havina makazi ndani yako.
🔰Ukiwa na uongo ambao unadhani utakuwa ni kweli utaficha hata kweli uliyokuwa nayo sasahivi. Kuna jambo unafanya lifanye kwa ukweli na sio lionekane la ukweli wakati unadanganya, hii inaweza kukufanya hata kupoteza yale machache ya ukweli uliyokuwa nayo.
🔰Kuna kuamka asubuhi na kujuta unapotoka mana hata inawezekana usiku ulikuwa unajisemesha bora kukuche, lakini nikwambie kitu ewe Mkristo na Muislamu mwenzangu ABRAHAMU katika Biblia alikuwa na imani kwamba Kunasiku atakuwa na familia yake na uzao wake lakini kabla ya kumpata Isaka Mungu alimwambia Uzao wake utakuwa kama mchanga wa Bahari, alimwambia Uzao wake Utakuwa kama nyota angani. Wewe leo hii unalala njaa au unalala sehemu ambayo hairidhishi lakini nawe kunasiku utakuwa zaidi ya matamanio ulikuwa nayo, kuna siku utakuwa na shibe zaidi ya njaa ambayo unayo leo, utakuwa na utajiri zaidi ya bajeti kali ambayo unayo kwa siku au mwezi au mwaka, Kumbuka Ayubu alivojaribiwa na shetani alipotezewa kila kitu lakini baada ya kushinda majaribu Alipata Mara mbili zaidi ya vya kwanza alivyokuwa navyo (Ayubu alionesha nidhamu,utii na Imani kubwa sana). Wewe kwani ni nani ambaye Mungu anakupa pumzi ya kuona changamoto za maisha na asikupe nguvu ya kuzishinda, wote tusimame na tuwe washindi. INAWEZEKANA.
Karibu kupata nakala yako ya NGUZO 3 ZA MAISHA kwa 10,000/= kujifunza zaidi.
📚Kwa Bei ya jumla ni 7500/= kwa vitabu 5 na kuendelea.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment