Habari mwanamafanikio katika mtandao wa Lazaro Samwel naimani u mzima wa afya na napenda kukupongeza kwa kuendelea kujumuika kuendelea kufuatilia application hii kwa ukaribu nikiwa naimani kwamba mwisho wa mwaka utakuwa na shuhuda kwa wengine juu ya mambo ambayo umeyapata katika application hii ya LazaroSamwel. Leo hii naomba tuende kwapamoja kuweza kueleweshana mambo kadha wa kadha kuhusu biashara ambayo unaifanya haijalishi biashara ya namna gani lakini iwe kwamba inatoa huduma kwa watu wako wa karibu na hata wa mbali ambao unawajua au huwajui katika sehemu mbalimbali.Kwanza napenda kuanza kukuliza kwasababu gani watu wengi husema kwamba biashara ni ngumu au inachangamoto? kwanini watu wanasema kwamba biashara hazilipi? Jibu kubwa ambalo utalipata ni kwamba wengi kufanya biashara ambazo haziwabebi wao lakini zinabeba waanzilishi wa biashara zile.Namaana gani kusema hivi? nasema hivi kwasababu watu wengi ni wavivu kufikiri na wanachokifanya ni kwamba kwasababu ya shida ambazo zinakuwepo hata kama anamtaji anaona ni bora nikafungua biashara kama mtu flani na sio kutokana na yeye alivyo kutokana na mawazo yake,hapa ndo tunasema kwamba unabebwa na biashara ya mtu mwingine na sio yako.Kunatofauti kubwa sana kati ya mtu kutembea na biashara ambayo kwanza kabisa yeye mwenyewe ni chimbuko wa wazo lile na kutembea na biashara ambayo wazo lake lake chimbuko sio wewe,naweza kusema kwamba kama wazo la biashara lingekuwa kama Application kwenye simu wewe ambaye unasema Application ni ya kwako utakosa uwezo wa kuupdate hiyo Application zaidi utakuwa unasubiri mmiliki afanye anachokijua kwanza ndipo na wewe uweze kufanya ulichoona.Wazo la biashara ambalo sio la kwako hauwezi kukua haraka kama wazo la biashara likiwa la kwako mana Penye chimbuko la wazo ndipo penye siri ya ukuaji wa biashara.Angalia ukitaka kuanza biashara sio unakurupuka kwenye mawazo ya watu,bora uteseke kwa miaka 20 au 10 unatafuta wazo la biashara ambayo itakufanya katika maisha yako yote usijutie kufanya biashara yako.
Changamoto katika biashara zipo na hatuwezi kusema kwamba hakuna changamoto.Lakini kunakitu flani ambacho ukikosea kabla ya kuanza kufanya biashara lazima changamoto zitazidi sana na utaona kwamba biashara yako haifai kabisa,ni kitu gani hichi? Ni kuharakisha kuanza kufanya biashara na kukimbia kufanya maandalizi ya biashara.Sehemu kubwa ambayo mtu unatakiwa kupanga biashara ni kwenye kufanya maandalizi ya kufanya biashara na sio kwingine kwasababu kwenye kujiandaa kufanya biashara ndipo ambapo tunatengeneza msingi mzuri wa biashara.Hapa utapata changamoto ambazo sio za kawaida na ukiruka katika sehemu hii hizo changamoto ambazo ulikuwa unatakiwa uzipate katika maandalizi ya kuanza biashara lazima utazipata wakati unafanya biashara.Usiache kujifunza nini kinatakiwa kifanyika katika biashara ambayo unataka kuanza.Usikurupuke tuu kwasbaabu ni msimu flani wa soko,hii misimu itapita lakini biashara yenye misingi imara itabaki na lazima pesa itatengenezwa na faida utaipata.
Naomba kuishia hapa na nakupongeza kwa kuchukua muda wako kusoma makala hii katika application hii ya Lazaro Samwel,hakikisha kwamba ujumbe huu hauishii kwako shirikisha na marafiki zako wadownload application hii ili wajifunze zaidi na zaidi.
Lazaro Samwel
CONTACTS ; 0753386586 / 0653386586
EMAIL ; lazarosamweli41@gmail.com
Youtube ; Lazaro Samwel
Facebook ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment