Tuesday, May 23, 2017

KWANINI TANZANIA INAWAKATI MGUMU KUJIKOMBOA

Tokeo la picha la TANZANIA FLAG QUOTES
Huwa nakaa na kutafakari ni kitu gani ambacho nchi yetu ya Tanzania imekosa mpaka sasa inakuwa tumeridhika na neno kwamba ni kati ya inchi masikini Duniani, yani watu kuishi chini ya kipato chao. Nilitafakari sana na nikawa na mawazo yafuatayo; 

1.Tanzania bado tunahali ngumu haswa kabisa kuanzia kwa viongozi ambao wanatuongoza, nasema hivi kwasababu wengi hawafanyi kazi kwasababu za kutoka katika mioyoni mwao ila wanafanya kwa asilimia kubwa kutokana na majukumu ambayo wanayo kibinafsi. Uongozi ambao hauna kusudi la wengi ila unakuwa na kusudi la mtu mmoja kwanza. Viongozi wengi wa Tanzania ni waongo ila hili jambo kinachukuliwa kama ni kawaida na mpaka imefika imekuwa kama tamaduni kwa viongozi.Kiongozi mwongo hawezi kufanikiwa katika mambo yake kama katika mambo ambayo anafanya anaweka uwongo, toka lini shetani ukimchanganya na jambo jema upate jambo jema? Hakuna hata siku moja ndomaana mafanikio ya Tanzania ni taratibu sana kwasababu walioshikilia mamlaka wanafunika uzuri wa mambo ambayo yangeweza kutokea kwa uwongo. Hakuna mafanikio yoyote ya kiongozi kama kila anachokifanya kinachembe ya uongo. Kunakitu ambacho watanzania tuanze kufunguka kwa kuangalie mbele zaidi, tusiangalie kiongozi kwa uzuri wa maneno ila tuangalie historia ya mtu ambaye anahitaji kuwa kiongozi kwa kipindi cha nyuma mpaka muda ule ambapo anataka kuwa kiongozi wenu ili tusije kuwa na viongozi ambao wanafanya kazi kwaajili ya uwongo na peda na sio kwaajili ya watu wao. 

✅Kiongozi unatakiwa kujua kwamba watu hawakuangalii kwa yale ambayo unayasema lakini kwa yale unayoyatenda.

✅Kiongozi lazima ujue ukifanya kazi kwaajili ya pesa lazima itasahau kufanya kazi kwaajili ya watu wako pia.


2. Tanzania inawakati mgumu kwasababu tumeshakubaliana na hali ya maisha ya kwamba hatuwezi kufanya jambo lolote kubwa na jipya mpaka watu wa njee waje,inaweza ikawa wachina au wamarekani au waingereza pia hao ndio ambao tunaamini kwamba wanaweza kufanya jambo vizuri, yani sisi tumejiweka kwenye kufanya mambo madogo tuu na ndo tunaona  uwezo wetu ulipo, ukitaka kuthibitisha hilo nenda kwenye kampuni alafu weka watu wawili mmoja mzungu na mwingine ni mwafrika mtanzania alafu sema tuu mtampa nan ajira? Bila kuangalia chochote asilimia kubwa watachagua yule mzungu kwasababu tayari wengi tumekuwa waathirika kifikra kuhusu sisi wenyewe,sio hivyo tuu watanzania sisi wenyewe bado tumewekeza katika chuki nikimaanisha vya nyumbani havithaminiwi kama vya njee vinavyothaminiwa. 
"Mtu mwenye ufinyu mdogo wa mawazo atasema Tanzania haina waandishi wazuri wa vitabu ikiwa yeye mwenyewe hanunui vitabu vya wenzake watanzania na kukazania vya njee tuu, mtu mwenye ufinyu mdogo wa mawazo atasema Tanzania ni masikini ikiwa kila siku yeye ni kusifia watu wa njee ikiwa kunawatu katika nchi yake wanafanya vizuri zaidi hata ya wa njee, mtu mwenye ifinyu mdogo wa mawazo yuko radhi kununua juice ambayo imetengenezwa  Marekani akaacha za Tanzania alafu anasema Tanzania masikini, mtu mwenye ufinyu mdogo wa mawazo atanunua supermarket vyakula vya njee akaacha vya watanzania wenzake na akasema Tanzania hakuna wajasiriamali wazuri".


Hizi ni sehemu mbili muhimu ambazo naweza kuchangia kwa kifupi tunaweza kusema kwamba chanzo cha Tanzania kutokusonga mbele ni ; 

1: Serikali ya viongozi.

2. Watanzania Wenyewe.
Chukua hatua angalia nafasi yako ni ipi jirekebishe. 

Karibu Sana Lazarosamwel Application Zidi kuinuka Mwaka huu. 

By Lazaro Samwel 
0753616584 / 0653387586 

Email ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment