Wednesday, May 24, 2017

USIWE MSINDIKIZAJI KATIKA MAHUSIANO AU NDOA YAKO.



 Tokeo la picha la relationship quotes about being a scotter in relationship
Kuna watu ambao wapo na wanavipawa vizuri sana lakini wanakuwa ni wasindikizaji wa kile kitu ambacho wanacho,kuna wengine ni wanawake wazuri nikimaanisha mke ambaye anaweza kuleta mabadiliko katika familia na ni mcha Mungu lakini mme anamtumia kama chombo flani katika familia,kuna wanawake wengine pia wana wanaume wazuri kitabia nikimaanisha kwamba wamemshika Mungu na wako tayari kupigana kwaajili ya faida ya familia nzima lakini bado mke katika familia unakuwa ni mkatisha tamaa kwa mme wake na anakuwa na roho ngumu ya kumpa moyo mme wako  katika shughuli zake za kila siku hata kama akiwa hana kitu kama yuko kwenye mashindano wakati na ndoa wamefunga na mmekula na kiapo kwa mungu wenu. Mwanamme au mwanamke katika familia usisindikize kipawa cha mke wako au mme wako kwasababu tayari mko naye kwenye ndo unatakiwa kuonesha uwepo kwa kuzidi kunawirisha kitu ambacho mwenzako anacho na sio kukipoteza.Itakuwa ni aibu kama unakuwa katika ndoa na mwenza wako na ndo unakuwa mdidimizaji mkubwa kwa upande wa mwenzako,hapo hauwezi kufika hata siku moja.Kuna watu ambao wanaingia katika ndoa wakiwa na mawazo ya kama kuna mashindano lakini kumbe ni kuonesha kukua kiumri na sio kiakili katika swala la ndoa.Ukifunga ndoa na mwenza wako jua umefunga ndoa naye  kwa kila kitu ambacho anacho na ndio maana ya kusema kwamba mnakuwa mwili mmoja na mnakuwa kama kitu kimoja  mana sifa ya kuwa kitu kimoja ni kwamba kwanza mnakuwa na mambo flani ambayo sio ya kujificha na sio ya utofauti baina ya mwenzako na kama mngekuwa na utofauti ambao hauna muunganiko na mwenzako hata msingeweza kufunga na ndoa pia.
 Tokeo la picha la relationship quotes about being a scotter in relationship

Usisindikize kitu ambacho unatakiwa kukionganisha nawe ili uweze kuwa mbali zaidi.Mfano kwa vijana tunausemi ambao wengi wameusikia unasema kwamba “Ujana ni maji ya moto” hatuwezi kukataa kwamba kijana ni maji ya moto lakini unasindikizaje hayo maji yako ya moto kwa manufaa yako ya baadae mana kunamwingine anasema kwamba ni maji ya moto akisindikizwa na maneno ya watu,vipi wewe mwenyewe baada ya kujua kwamba Ujana kweli ni maji ya moto umefanya jambo gani kuweza kuleta matokeo mazuri ya maandalizi ya maisha yako ya ndoa? Au umekuwa maji ya moto ambayo hayana maarifa wala hekima ya kujitambua na kila sehemu unaona ni kutumia hali yetu ya kuwa moto kushusha hadhi zetu? Nafasi yako sio ya kusindikiza lakini kuungana na Yule ambaye unawaza kumsindikiza na hapo ndipo unapoweza anza kuona mabadiliko makubwa katika kila jambo ambalo unalifanya na mwenza wako.


Lazaro Samwel
Contacts ; 0753616584 / 0653386586
Email      ; lazarosamweli41@gmail.com

Youtube  ; Lazaro Samwel
Facebook; Lazaro Samwel 

0 comments:

Post a Comment