"Ukitembea katika kusudi lako lazima fikra zako zibadilike na kuwaza mambo sahihi" -Lazaro Samwel
Mungu aliamini kwamba kumpa binadamu kusudi ndiyo njia pekee ya kuweza kumsaidia kupambana na shetani kwasababu binadamu hataweza kufanya mambo maovu akiweza kutambua kusudi lake. Naye shetani akaona njia pekee ya kumkomoa Mungu japo haiwezekani ni kuhakikisha kwamba anafunga ufahamu wa binadamu kujua kusudi lao.
Norman Vincent Peale alishawahi kusema "Empty pockets never held anyone back. Only empty heads and hearts can do that" akimaanisha kwamba " Mfuko mtupu hauwezi kumrudisha mtu nyum.Ni akili tupu na moyo mtupu unaweza fanya hivyo".
Amini katika kila jambo ambalo unalifanya ukigusa maisha ya watu wengine Mungu hawezi kukuacha bure.Kumbuka sio lazima upate hela ndipo useme nimepata baraka za Mungu kwasababu wengi wanadhani mafanikio au baraka kutoka kwa Mungu kwa kusaidia wengine ni hela.Kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya na usiona matokeo makubwa sana ila ukawa na maisha ya kawaida yenye furaha sana hii pia ni mafanikio. Ila baraka zake kizazi chako au watoto wako ndio ambao wanakuja kupokea baraka hizo za wewe kusimama katika kusudi lako la kusaidia wengine.
Wewe kuwa na furaha ya kuweza kusaidia watu wengine kuwa na furaha na kufanikiwa hiyo kwako pia ni mafanikio kwamaana kuna watu wanatafuta hiyo furaha hata kidogo hawaioni ila wewe unawasaidia kuwatoa katika janga hilo. Mungu anaweza kukuleta duniani ili utengeneza maisha bora ya kizazi chako kijacho, yani wewe unakuwa kama muandaaji wa kizazi chako au vizazi vingine.Kuna mwingine ameletwa duniani kuinua wengine na wawe na maisha ya juu sana.Wewe kufanikiwa katika kusudi lako sio lazima wewe unifaike nalo kwa sasahivi ila hata kizazi chako kinaweza kuonesha kwamba wewe ulifanikiwa kutimiza kusudi lako, usifikiri kwamba kusudi liko kwenye hela tuu,hapana. Kumbuka ukitembea katika kusudi lako matokeo yake unaweza usione sasahivi zaidi ya kuona ishara za mafanikio,lakini jitahidi kuendelea kufanya kitu ambacho akili na roho yako inakutuma kufanya bila kukiuka matakwa ya Mungu.
Lazaro Samwel
0753616584 / 0653386576
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment