Kwanza kabisaa ningependa kukwambia kwamba ukiwa katika mfumo ambao hauumiliki ni ngumu sana kuweza kupiga hatua ambazo unazihitaji katika maisha yako. Haswa pale unapojua kwamba hata kama ukiongeza juhudi namna gani bado utakuwa palepale katika kiwango cha kipato ambacho utakipokea. Tunaweza kusema kwamba utakuwa unaishi kutokana na mashariti ambayo mfumo unakuhitaji kuishi nao, ndo maana tunasema kwamba tunakuwa hatuna uhuru katika kuwa na maamuzi kwenye ajira ambazo unakuta umeajiriwa.Hii ni dhahiri kwamba sio kila mmoja anafanya kazi kwa kupenda lakini wengi wanafanya kazi kwa kupenda hela na sio kupenda kazi ambayo wanaifanya ndo maana hata maendeleao yanakuwa madogo sana mfano kwa uchunguzi ambao ulishafanyika kule Scotland kwa miaka 10 ulionesha kwamba 10% ya watu hupoteza maisha yao asubuhi jumatatu kutokana na kufanya kazi ambazo hawazipendi, hii inamaana gani? Ni kwamba hata maisha ya mwajiriwa huwa hayana uhuru na wala hayana raha sana pale kunapokuja kuweka maamuzi njee na mfumo ambao anao. Nilishawahi kusema kwamba mwajiriwa usijisahau ukiwa kwenye ajira mpaka ukaona wewe ndo mwajiri ila jaribu kukumbuka kwamba mambo yafuatayo katika ajira ambayo unayo au unategemea kuwa nayo;
1. Kunamambo yako binafsi ambayo unatakiwa kuyafanya tena ikiwezekana iwe ndo mkombozi wa kukufanya wewe uanze kula matunda mazuri ya pension yako ukiwa katika umri mdogo ambao unaweza kuendelea kujitengenezea mazingira mengine mazuri ya kugusa jamii na dunia kabisa. Hapa pia inabidi uangalie mambo mengine ambayo kweli ndipo kusudi lako lilipo mana muda mwingine itakuhitaji wewe kufanya kitu ambacho hukipendi kupata kitu ambacho unakipenda. Usijisahau kijana mwenzangu kwa hili, uliumbwa kumiliki mfumo na sio mfumo kukumiliki wewe.
2. Kumbuka pia utakuwa na familia na mshahara wako hauwezi kujitosheleza kuhakikisha kwamba watoto wako wanasoma shule nzuri au kuvaa na kufanya mambo mengine mazuri ya maendeleo (Rejea no.1) lazima ujiongeze, usiridhike na uzuri wa majengo ya pale unapofanyia kazi ukadhani kwamba imefika, usiridhike na AC za ofisi pamoja na gari la ofisi ambalo huwa linakubeba muda mwingine, jua ukistaafu haya mambo yote hayatakuwepo yani utayaacha nyuma utaenda kwako, je wewe utakuwa na kitu gani zaidi ya hivyo? Watoto wako watasema nini kuhusu kutumia ujana wako kutengeneza kesho yao? Chukua hatua ndugu hapo ulipo sio pa kukaa milele jua kunamoto ambao huwa unawaka sana ndani yako kuhusu kufanya jambo flani lakini unaogopa kwamba jamii itakuelewaje ukiacha ajira, au mke wako au mme wako atakuelewaje kama utaacha ajira? Hey Mungu alikuumba utawale na sio utawaliwe kama vile wana wa Israel walivyotoka Misri licha ya kuwa watumwa kwa muda mrefu lakini bado ni taifa teule la Mungu hata wewe bado u taifa teule la Mungu katika kubadilisha maisha yako.
Unapata picha gani unaposikia serikali ya Tanzania imefukuza wafanyakazi zaidi ya 9000 lakini hawa wote hawana kauli yoyote juu ya serikali? Na hawa wamefanya kazi kwa muda mrefu licha kuwa na makosa? Inamaana hata wewe ambae bado upo kazini bado hauna sauti japo unaona unasauti flani, ningependa kukushauri hata kama una kazi ya manager, kwenye taasisi yoyote hakikisha akili yako inawaza wewe flani utafanya nini ili uwe CEO siku moja katika taasisi yako!? Wewe unaogopa kuwa kama unavoona unaweza kuwa kwasababu ya ajira lakini unaweza kuwa zaidi ya ajira uliyokuwa nayo ndo maana hata picha ambayo unataka kuwa unaiogopa mana unakuwa na maswali mengi kama itatimia au vipi? Mwisho wa siku unaona ni bora tuu uteseke lakini upate hiyo hela ya kawaida tuu. Inawezekana kubadili maisha yako, tumia ajira uliyokuwa nayo kutengeneza ajira zako mwenyewe na uwe na kauli na uhuru wa kufanya maamuzi. Unastahili kuanza kula faida za ujana wako ukiwa bado na umri mdogo sana kama kweli utaamua kuthubutu katika maisha yako.
Kunamaisha flani ambayo unastahili kuishi zaidi ya sehemu uliyoko katika maisha yako mpenzi msomaji katika application ya Lazaro Samwel ni muda wa kuchukua hatua na sio kuogopa na kujiona unapaswa kukaa hapo ulipo katika maisha yako.
Ulikuwa nami;
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook ;Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment