Kuomba Msamaha
Habari Wapendwa,
Hongera sana kwa kuendelea kufuatilia Application hii,umeshawahi kujiuliza nini maana ya EGO? Hebu twende pamoja na Mr Robert Reuben kwenye somo hili;
EGO ubinafsi umo, kujiona bora kuliko mwingine, kutokujali wengine zaidi, kujiona bora kuliko mwingine, kuangalia maslahi binafsi tu nk mfano Sasa hayo yote ukipata mtu ana pesa, elimu cheo, umaarufu nk na akwa hajielewi ndipo inakuwa balaa, mfano mwingine Ni kama kujifutua fulani hivi, kuona "kwani utaniambia nini, utanifanya nini. ..nk"
Naomba tuitafari Ego kwa mapana yake.
Kati ya vitu vinavyotafuna ndoa kwa haraka sana sio tatizo lililotokea, bali ni Ego ambayo inakuja baada ya tatizo kutokea....
Chukua mfano wa huyo dada kwenye hiyo video clip.... kilichomponza sio lile kosa, bali ni reaction yake baada ya kosa kutokea.
●Ego inaondoa UPENDO...
●Ego inaondoa UTII....
●Ego inaondoa KUHESHIMIANA NA KUSIKILIZANA...
●Ego inawaweka "mbali" wanandoa....
●Ego inakaribisha mawakala wabaya kuvamia ndoa... Nk nk.
Kwa ujumla, EGO ndio INAHARIBU NDOA pamoja na mahusiano mengi sana - haswa kwa vijana...
Huwa inapungua kutokana na umri unavyoongezeka. Ndio maana kesi za wanandoa waliovuka miaka 25, kuachana (kuondoa kifo) ni chache kulinganisha na vijana.
Ila KWA MTU MAKINI ANAYEJITAMBUA NA KUJIELEWA VIZURI, ANAWEZA KUI-CONTROL EGO YAKE HATA AKIWA NA UMRI WA CHINI YA MIAKA 30 NA AKAKUA NAYO HADI UZEE.
Tambua kuwa Ego inatoa PICHA PANA ya ukomavu mtu (maturity). Na hapa sizungumzii umri..... Jaribu kuchunguza; aliyekomaa vizuri Ego itakuwa chini (huyu ataongozwa zaidi na busara) na ukiona mtu analeta sana Ego.....
Kwa uzoefu wangu, matatizo yaliyomo ndani ya ndoa na mahusiano yetu, nathubutu kusema kwa zaidi ya 75%, yanasababishwa na hili jinamizi la EGOCENTRIC ....
Mara zingine utakuta tatizo lilishakwisha ila EGO ndio inaliendeleza kwa kusambaza sumu taratibu na kuleta matokeo yanayochukiza duniani mpaka mbinguni.
Ego zipo za aina nyingi: pesa, nguvu za mwili, elimu, cheo/mamlaka, kujulikana na viongozi wakubwa, umaarufu, historia nk..
Watu kujishusha tumeitafsiri vibaya, na matokeo yake kutaka kuonyesha viburi vyetu ndio kunatawala na kuleta madhara.
Ndugu zangu, viumbe karibu wote wana viburi ila tunapishana viwango na namna ya kuviamsha...
Ni kama uamue kumkomoa samaki kwa kumsukumia ndani ya maji....... Tumia kanuni hiyo hiyo kabla hujaamua kumfanyia kiburi kiumbe mwenye pumzi....
Naomba nimalizie kwa kusema:
<b>"kujishusha sio dalili ya unyonge, bali inaonyesha UKOMAVU NA BUSARA". /b>
"I AM SORRY": Maneno matatu yanayoweza kuokoa ndoa.
"EGO": Herufi 3 zinazoweza kuharibu ndoa.
Robert Reuben,
Author & Marriage Consultant.
23 May 2017.
<
0 comments:
Post a Comment