Tuesday, October 3, 2017

BADILI AKILI,ONA FURSA,BADILISHA MAISHA YAKO.

Image result for MISTAKES PICTURES



Ukiona kitu kimoja kinagombaniwa na watu wengi kupita kiasi jua Kuna mambo mawili yanakosekana kwa watu hao;

1.kujitambua.

2.Kujikubali.

®Ukijitambua utajiweka katika nafasi nzuri ya kujua kusudi lako ni lipi na wapi unapaswa kuwa  na hakuna mtu anayeweza kugombania kusudi lako hata kama wakigombania hawawezi kukunyang'anya.

®Ukijikubali utajua thamani ya ulichonacho na utasimamia kukikuza ulichonacho na sio kugombani kuwa kama wengi wanavyoshindana kuwa.

Sponsored by ; AKILI YA YA USHINDI (TOLEO LA 1&2)

Usipokubali kufanya makosa usitegemee kukua katika jambo lolote unalotaka kulifanya.Kuna watu Leo hawajafanya mambo makubwa na yenye kuwatambulisha kuishi katika kususi lao kwasababu wanatafuta ukamili WA kufanya mambo yao kwa kufanya mambo ambayo sio wao, nani kakwambia kuwa kamili unakupa asilimia zote kufananikiwa katika jambo lako? Usipoanza safari ya unapotaka kwenda hauwezi hata kuona Barabara ya unapoelekea mfano ikiwa ni usiku upo kwenye safari na unataka kufika kwako je utaogopa giza kwasababu ukiwasha taa za gari lako zinaishi mita kadhaa  kwa mbele na hauoni zaidi ya mwanga unapoishia? au utasonga mbele na kadri unavyozidi kwenda unazidi kuona mbele zaidi ya unapoenda? Naimani utasonga mbele na hautasema nasubiri mwaga WA asubuhi au kusubiri usafiri wa mtu mwingine. Wengi huwa tunasubiri usafiri wa watu wengine na hujikuta tuko sehemu ambayo sio kwasababu ya kutokuamini kwamba ili kufika sehemu tunayotaka ni lazima ukubali kusogea na usafiri wako. Maisha yako ni kama safari cha msingi ni kuwa na maandalizi ya usafiri wako na kusonga mbele usiseme nasubiri mwanga wa asubuhi au unasubiri usafiri wa watu wengine utachelewa unapotaka kwenda.

Nataka kukwambia kitu kimoja muhimu sana katika kufika au kupata kitu unachokitaka katika Maisha yako.Kumbuka haitakuwa kitu rahisi kujua kusudi lako kama unavyodhani na wala usijipe moyo utaweza kujua kusudi lako ukiwa umekaa kwako na kuangalia TV au kusoma magazeti ya udaku,kuna kujitambua na kujikubali,hivi ni vitu viwili vya mwanzo kabisa kwa MTU kugundua kusudi lake lakini angalia wangapi wako katika mambo haya mawili? Ni wachache sana angalia wasomi wanasoma nini na mwisho wa siku wanaishia kufanya nini? 99% of people are not aware of who they are.Maisha ya watu wengi yametawaliwa uwoga;

~Uwoga wa jamii itanionaje nikiwa mimi?.

~Uwoga wa baba au mama atanionaje nikimwambie napenda kitu flani kufanya?.

~Uwoga wa kufeli kwa  unachokipenda kukifanya.

~Uwoga wa marafiki zangu watanisemaje nikianza kufanya nachokipenda?

Jibu ni moja ANZA KUWA WEWE LEO narudia kukwambia ANZA KUWA WEWE LEO.

Kitabu cha Joel Osteen BECOME A BETTER YOU ukurasa wa 99 sehemu ya 8 (LEARNING TO LIKE YOURSELF-JIFUNZE KUJIPENDA MWENYEWE) paragraph  ya 3 mstari wa 1anaseme "Kitu kimoja kibaya ambacho unaweza kukifanya ni kuishi Maisha ambayo yanapingana na wewe".

Acha mambo ya kufanya kitu kuridhisha watu flani,  acha kuwa mtumwa wa kiu ya watu wengine. Kuna watu mpaka Leo wanaishi ndoto za wazazi wao na sio ndoto zao,Kuna watu mpaka Leo wanaishi ndoto za wazee wao na sio wao,Kuna watu wanaishi ndoto za marafiki zao na sio zao,Kuna wanaishi ndoto za jamii zao na sio zao. Huu ni utumwa mbaya sana katika Maisha yako,naweza kusema hauna tofauti na roboti. NI MUDA WA KUAMKA NA KUSEMA BASI NATAKA MAISHA YA NDOTO YANGU.Unajua Kuna muda unaweza kusema Mungu amekusahau lakini kumbe wewe ndiye kisababishi cha kushindwa kupokea Baraka zake,amekupa shamba lakini unashindwa kulilima na unaenda kulima kwenye mashamba ya watu wengine. Utasubiri sana maisha unayoyatamani kama Unaogopa kuumia au kulipa gharama katika mambo yako binafsi ya kukukuza na unaamua kufanya mambo ya watu wengine ili uepuke maumivi flani katika maisha yako.Usipende kuwa wa kawaida mana ukawaida utakufanya kuwa mtumwa kwa wale ambao wameamua kuwa zaidi ya kawaida.

Hakuna mafanikio bila gharama flani ya maumivu,nioneshe ambaye hajapata maumivu au changamoto yoyote ya mafanikio yake nami nitakuoneshe mafanikio yake yasio na uhalali.Hata mwizi anapata changamoto na hata kipondo kikali muda mwingine mpaka kuja kupata anachokitaka akibahatika kutoroka😀. Hata aliyeridhishwa utajiri na wazazi wake anapataa changamoto na maumivu kukua zaidi ya pale alipoachwa.Usipende virahisi utaishiwa kuwa rahisi sana kupoteza thamani yako kwa wale wanaojua thamani zao.

Hebu nikuache na swali hii maana hapa sitamaliza;

®Jiulize unachokifanya Leo unakipenda? Kama HAPANA unasubiri nini kubadilika? na kama NDIO kwanini Maisha yako hayabadiliki au kwanini hutaki kukua zaidi ya hapo?

®Kitu gani unachopenda kufanya?
Kama kipo kwanini unagopa kuanza? Kama unaogopa watu kwani wanajua haya unachowaza,au kwani wao ndio wenye kusudi lako? Kama hapana ANZA LEO UNACHOKIPENDA na ENDELEA KUJIFUNZA.

🔎TO BE A SUCCESSFUL PERSON YOU MUST BE ABLE TO CONQUER YOUR FEAR TO DO MISTAKES THEN ALLOW YOURSELF TO LEARN FROM YOUR MISTAKES.

Kuwa na Wakati Mwema.

Jiunge na Program ya AKILI YA USHINDI kwa kubonyeza http://www.akiliyaushindi17@gmail.com/jiandikishe/

Ulikuwa nami;

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
Email; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment